Friday, August 08, 2025

BALOZI NCHIMBI ATOA POLE KIFO CHA SPIKA MSTAFAU JOB NDUGAI







Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametembelea nyumbani kwa marehemu Mhe. Job Yustino Ndugai, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kilichopo Mtaa wa Njedengwa jijini Dodoma, kutoa salamu za rambirambi kufuatia kifo chake.

Akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, Balozi Nchimbi alitoa pole kwa mjane wa marehemu, Dkt. Fatma Mganga, pamoja na familia na ndugu waombolezaji waliokusanyika nyumbani hapo leo Ijumaa, tarehe 9 Agosti 2025.

Katika ziara hiyo, Balozi Nchimbi pia alisaini kitabu cha maombolezo na kuungana na wafiwa katika kipindi hiki kigumu, akieleza kuwa kifo cha Mhe. Ndugai kimeacha pengo kubwa katika uongozi na historia ya Bunge la Tanzania.

No comments:

TUZINGATIE UTU, SHERIA NA HAKI KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA ULINZI WA RASILIMALI ZA TAIFA- DKT KIJAJI

  Na. Joyce Ndunguru, Morogoro. Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Dkt Ashatu Kijaji (Mb) amewataka watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa W...