Tuesday, August 05, 2025

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ashiriki Kupiga Kura ya Maoni Jimbo la Ruangwa

 




Ruangwa, Lindi – Agosti 4, 2025

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), ambaye pia ni aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ruangwa kwa vipindi kadhaa, leo ameshiriki zoezi la kupiga kura ya maoni za kuwapata wagombea wa nafasi ya Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025.

Zoezi hilo limefanyika katika Kata ya Nandagala, nyumbani kwa Waziri Mkuu, ambapo alijitokeza mapema katika kituo cha kupigia kura kilichopo ndani ya kata hiyo, huku akipokelewa kwa heshima kubwa na wananchi pamoja na viongozi wa chama katika ngazi ya wilaya na mkoa.

No comments:

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AMWAKILISHA WAZIRI WA FEDHA KATIKA KONGAMANO LA 16 LA MWAKA LA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI – ARUSHA

Naibu Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Mhandisi Mshamu Ali Munde, amemwakilisha Waziri wa Fedha katika ufunguzi wa Kongamano la 16 la Mwaka la Wa...