OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAANDAA WARSHA YA UZINDUZI WA MRADI WA KUJENGA UWEZO KWA TAASISI KATIKA UDHIBITI WA KEMIKALI NA TAKA SUMU
Mgeni
Rasmi katika warsha ya uzinduzi wa Mradi wa kujenga uwezo kwa Tasisi
katika udhibiti wa kemikali na taka sumu , Bwana Richard Muyungi ambaye
ni Mkurugenzi idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais akiongeakatika
uzinduzi wa warsha hiyo.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Magdalena
Mtenga akiongea wakati wa warsha hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu
wa Rais, Idara ya Mazingira.
Sehemu ya Washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi (hayupo pichani).
Mwakilishi
wa UNEP Bibi Nalimi Sharma akiongea katika warsha hiyo, pembeni yake
Mkurugenzi wa Mazingira Ofsis Ya Makamu wa Raisambaye ni Mgeni Rasmi
Bwana Richard Muyungi
Mkurugenzi
wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi akiwa katika
picha ya pamoja na Wajumbe waliohudhuria warsha hiyo kutoka Taasisi
mbalimbali za Serikali.
Nchi
zinazoendelea zinakabiliwa na changamoto katika suala zima la usimamizi
na udhibiti wa kemikali na taka sumu. Taka sumu nyingi zimekua tishio
kwa Wananchi hasa Wanawake na Watoto.
Hayo yamesemwa na Mgeni Rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Bwana Richard Muyungi alipokua akifungua warsha ya uzinduzi wa mradi wa kujenga uelewa kwa Taasisi za Serikali katika udhibiti na usimamizi wa kemikali na taka sumu jijini Dar Es Salaam.
Hayo yamesemwa na Mgeni Rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Bwana Richard Muyungi alipokua akifungua warsha ya uzinduzi wa mradi wa kujenga uelewa kwa Taasisi za Serikali katika udhibiti na usimamizi wa kemikali na taka sumu jijini Dar Es Salaam.
Pia
ametoa shukrani kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) kwa
msaada wa kifedha katika kuanzishwa kwa mradi huo, ameongeza pia
Wajumbe waliohudhuria warsha hiyo wakaitumie vema elimu watakayoipata
katika sehemu zao za kazi ili kuongeza weledi na maarifa.
Akiongea
katika warsha hiyo Mwakilishi kutoka UNEP Bi.Nalimi Sharma amesema
amefurahi sana kuhushuria uzinduzi wa warsha ya mradi huo na kuona
jitihada mbalimbali zinazochukuliwa katika suala zima la usimamizi na
udhibiti wa kemikali na taka sumu. Ameongeza kuwa UNEP itaendelea kutoa
msaada wa kifedha kwa kwa Ofisi ili kuendelea kuimarisha shughuli za
usimamizi na udhibiti wa kemikali na taka sumu.
Comments