Monday, October 09, 2017

WAANDISHI WA HABARI WASHAURIWA HABARI ZA VIJIJINI


Waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali wakiwa katika mafunzo ya uandishi wa habari za vijijini mkoani Morogoro ,Semina hiyo imeratibiwa na umoja wa vilabu vya habari Tanazania(UTPC).
Mwezeshaji wa semina Joe Nakajumo akifundisha katika mafunzo hayo leo Mkoani Morogoro.
Kushoto ni Noria Damian ,katikati Editha Carlo pamoja Happines Mtweve wakifatilia mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari za vijijini wakifatilia mafunzo hayo kwa ukaribu
Amon Mtega kutoka Ruvuma Press club akiachangia mada katika mafunzo hayo ,kulia ni Queen Isack kutoka Kilimanjaro Press Club
Kushoto ni mwakilishi kutoka Arusha Press club Pamela Mollel,katikati ni Adam Juma kutoka Mtwara Press Club wakifuatilia mafunzo hayo.
Mwandishi wa habari Laudence Simkonda kutoka Mbeya kulia Oscar Simon kutoka Rukwa wakifuatilia mafunzo hayo.

Na Pamela Mollel,Morogoro

Waandishi hapa nchini wameshauriwa kuongeza muamko katika kuandika na kutangaza habari za vijijini kwa kuwa asilimia 75 ya wananchi wa Tanzania wanaishi vijijini, ambako wanaendesha maisha yao kwa kufanya shughuli mbalimbali

Rai hiyo imetolewa leo Mkoani Morogoro na mwenzeshaji Joe Nakajumo katika mafunzo ya uandishi wa habari za vijijini iliyowakutanisha wanahabari kutoka mikoa mbalimbali iliyoratibiwa na umoja wa vilabu vya habari Tanazania (UTPC).

Nakajumo alisema kuwa waandishi wa habari wanajukumu kubwa la kuwa karibu na jamii ya vijijini kwa kutambua shughuli zao wanazozifanya na kuzifatilia kwa kuona mafanikio yao pamoja na kuibua kero zinazowakabili

“Asilimia 75 ya wananchi wanaishi vijijini wanaendesha maisha yao kwa kufanya shughuli za kilimo,ufugaji ,uvuvi,ujasiriamali hivyo ni muhimu sana  kuwapa kipaumbela wananchi hawa”alisema Nakajumo.Aidha alisema kuwa moja ya majukumu ya msingi ya mwandishi wa habari ni kusaidia na kushiriki katika ujenzi wa taifa hivyo anapaswa kuudhihirishia umma kwa watu wote nchini wanapaswa kupata habari

Kwa upande wake mshiriki wa semina hiyo Adam Juma alisema kuwa mafunzo haya yatasaidia kuibua changamoto vijijini ambako panaoneka kusaulika kwa huduma mbalimbali za kijamii.Pia aliwaomba waandaji wa semina hii UTPC kuendeleza mafunzo haya kwa waandishi wa habari ili kuweza kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya taaluma hiyo

Umoja wa vilabu vya habari Tanazania(UTPC)imekuwa ikiendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa waandishi wa habari lengo ikiwa kuwaongezea ujuzi wa kufanya kazi zao kwa kufata misingi ya taaluma .

No comments: