Zoezi
la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Wilayani ya
Ukerewe likiendelea, pichani ni baadhi ya wananchi wa kata ya Kakelege
wakisubiri zoezi la kupigwa picha na kuchukuliwa alama za Kibaiolojia.
Afisa
Usajili Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Ndg. Zabron Rusohoka
akiwaelekeza baadhi ya wananchi taratibu wanazopaswa kuzifuata wakati wa
ujazaji fomu za maombi ya Wilayani Ukerewe.
Umati
wa wananchi wa Kata ya Ukerewe kijiji cha Nakatunguru wakisubiri huduma
ya Usajili wakati zoezi la Usajili likiendelea Wilayani humo.
Mmoja wa mafafisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa akimsaidia mmoja wazee waliofika kwenye kituo cha usajili kusajiliwa.
Mwananchi wa kata ya Nansio akichuliwa alama za kibaiolojia wakati wa zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa
Hawa
ni baadhi ya akinamama wa Kituo cha Nansio Ukerewe waliojihimu mapema
kusajiliwa wakati zoezi la usajili likiendelea Wilayani humo.
………………
Usajili
Vitambulisho vya Taifa katika mkoa wa Mwanza na wilaya zake umepamba
moto, ambapo wananchi kutoka Wilaya za Kwimba, Ukerewe, Ilemela,
Misungwi na Sengerema wamejitokeza kwa wingi kusajili. Kwa wananchi wa
Wilaya Nyamagana, taratibu za kuanza kwa Usajili zinaendelea ambapo
wataanza usajili rasmi wiki hii.
Katika
kufanikisha zoezi hilo Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa
Halmashauri na Manispaa pamoja na Watendaji wa mitaa/Vijiji wamejizatiti
kwa dhati kuhakikisha zoezi hili linafanyika na kukamilika kwa wakati
uliopangwa. Aidha; Wamewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kusajiliwa
kutokana na manufaa mapana ya zoezi hilo kwa mwananchi mmoja mmoja na
kwa Taifa kwa ujumla.
Comments