Airtel yasherehekea wiki ya huduma kwa wateja kwa kuzindua OFA KAMBAMBE


Meneja wa duka la Airtel Makao Makuu Bi Celine Njuju akiongea na wateja leo wakati Airtel ilipozindua wiki ya huduma kwa wateja pamoja na kuzindua kifurushi cha OFA kabambe kinachopatikana kupitia Airtel Money kwa shilingi 1000 tu na kudumu kwa siku 3. kifurushi hiki pia kinampatia mteja GB 2, dakika za maongezi 110 kwenda mitandao yote pamoja na sms bila kikomo uzinduzi wa wiki.

Katikati ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba akikata keki kuashiria uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja inayoazimishwa duniani kote kuanzia octoba 2 hadi oktoba 6 huku akiwa amezungukwa na baadhi ya wafanyakazi wa Airtel pamoja na  wateja wa Airtel waliotembelea duka la Airtel Moroco kujipatia huduma.
 Mmoja kati ya wateja wa Airtel Bw, Kassim Nguya akimlisha keki Mkurugenzi wa huduma kwa mteja Bi Adriana Lyamba maalum kwa kuashiria uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja ambayo huanzimishwa kila mwaka mwezi oktoba tarehe 2 hadi 6. airtel pia imezindua kifurushi cha OFA kabambe ambapo kwa  shilingi 1000 mteja anapata  GB 2, dakika za maongezi 110 kwenda mitandao yote pamoja na sms bila kikomo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Airtel huduma kwa mteja  wakiwa tayari kuwakaribisha wateja na kuwahudumia.

 Baadhi ya wateja wa Airtel waliotembelea duka ya Airtel Makao makuu leo wakilishwa keki na Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba leo ikiwa ni kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja inayoazimishwa duniani kote kuanzia octoba 2 hadi 6. Airtel mwaka huu wamesherehekea wiki hio wakiwa na kauli mbiu yao ya BUILDING TRUST yaani kuwajengea wateja Imani kwa kuwapatia huduma zenye viwango. 


Airtel leo wamezindua shamra shamra za wiki ya huduma kwa mteja kwa kuwakaribisha wateja wake wote waliongia madukani kwao kwa kukata keki na kuzindua kifurushi maalum cha sh 1000 cha OFA KABAMBE kinachodumu kwa siku tatu ikiwa ni ishara yakuwashukuru wateja wote nchini. 

 Akiongea katika makao makuu ya Airtel Meneja wa Duka la Airtel Bi Celine Njunju alisema “tunawashukuru wateja na wananchi wote kwa ujumla katika wiki hii ya huduma kwa wateja inayoanza tarehe 2 hadi tarehe 6 mwezi Oktoba duniani kote, kwa upendo kabisa Airtel inakupa kifurushi cha OFA KABAMBE kupitia Airtel Money kitakachokupa uhuru wa kujichagulia kile unachokipenda kutoka Airtel”. 

 Ukijiunga na Ofa kabambe ya Airtel Money, kwa Tshs 1000 tu! utapata GB 2, Dakika 110 za kupiga mitandao yote na SMS bila ya kikomo, huku ukiwa na uhuru wa kutumia kifurushi hiki ndani ya siku tatu toka pale ulipo nunua. Alieleza kuwa “ili kujiunga Piga *150*60# chagua 6 kufurahia vifurushi vinavyokupa MB na Dakika kibao pamoja na SMS bila ya kikomo” “uhuru ni wako tumia utakavyo ndani ya siku tatu.

Alisisitiza Bi Celine kwa upande wake Mkurugenzi wa kitengo huduma kwa wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba alieleza kuwa “ wiki hii huadhimisha kila wiki ya kwanza ya mwezi oktoba kila mwaka, lakini kwetu Airtel kila siku tunazingatia swala muhimu la kutoa huduma kwa wateja wetu wote kwa viwango vinavyotakiwa

 “Mwaka huu Airtel tumeipa wiki hii kauli mbiu Building Trust tukimaanisha kuendelea kuwajengea wateja wote Imani katika huduma tunazotoa” alieleza Bi Lyamba . 

 Bi Lyamba aliendelea kusema “wiki hii pia Airtel tutakuwa na matukio mengi maalumu kwa wateja wetu lakini muhimu zaidi tunawakaribisha wote mtembelee katika ofisi zetu za huduma kwa wateja ili muendelee kujipatia huduma bora kama vile kusajili laini mpya, kujipatia simu na vifaaa vya mawasiliano original kwa bei nafuu na vitakuwa na ofa kabambe maalum kwa ajili yako, pia utaelekezwa jinsi yakutumia huduma zetu kama Airtel Money, Airtel Yatosha, huduma ya kukopa kwa Airtel Money yaani Timiza na nyingine nyingi

Comments