Meneja wa Benki ya NBC Tawi la
Mbagala, Sady Mwang’onda (wa pili kulia)
na Meneja Bidhaa za Uwekezaji wa benki hiyo, Dorothea Mabonye (wanne kushoto),
wakikata utepe kuashirikia uzinduzi rasmi wa kampeni ya akaunti ya malengo ya
NBC. Kampeni hiyo itakayodumu kwa muda wa miezi mitatu na kufanyika nchini kote
itashuhudia washindi sita wakijishindia kila mmoja gari jipya aina ya Suzuki
Carry ‘kirikuu’ lenye thamani ya shs milioni 30. Washindi wengine 24 watajishindia
kila mmoja zawadi ya pesa taslimu shs milioni moja hivyo kufanya jumla ya
zawadi zote kufikia thamani ya shs milioni 204. Hafla hiyo ilifanyika katika
tawi hiyo, Dar es Salaam leo. Wengine ni baadhi ya maofisa wa benki hiyo.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la
Mbagala, Sady Mwang’onda (katikati),
Meneja wa Bidhaa za Uwekezaji wa benki hiyo, Dorothea Mabonye (kulia kwake), na
Mkuu wa Bidhaa na Wateja Rejareja,
Andrew Lyimo (kushoto kwake), pamoja na baadhi ya maofisa wa benki hiyo
wakishangilia mara baada ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya akaunti ya malengo ya
NBC uliofanyika katika tawi hilo, Dar es Salaam leo. Kampeni hiyo itakayodumu
kwa muda wa miezi mitatu na kufanyika nchini kote itashuhudia washindi sita
wakijishindia kila mmoja gari jipya aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ lenye
thamani ya shs milioni 30. Washindi wengine 24 watajishindia kila mmoja zawadi
ya pesa taslimu shs milioni moja.
Mkuu Bidhaa na Wateja Rejareja
wa Benki ya NBC, Andrew Lyimo (katikati), akihojiwa na waandishi kutoka vyombo
mbalimbali vya habari mara baada ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya akaunti ya
malengo ya NBC uliofanyika katika tawi Mbagala nje kidogo ya Jiji la Dar es
Salaam leo. Kampeni hiyo itakayodumu kwa muda wa miezi mitatu na kufanyika
nchini kote itashuhudia washindi sita wakijishindia kila mmoja gari jipya aina
ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ lenye thamani ya shs milioni 30. Washindi wengine 24
watajishindia kila mmoja zawadi ya pesa taslimu shs milioni moja.
Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria
Kimaryo akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya akaunti ya
Malengo ya benki hiyo, Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Meneja wa
tawi la Mbagala, Sady Mwang’onda, Meneja wa Bidhaa za Uwekezaji, Dorothea
Mabonye, Mkuu wa Bidhaa na Wateja Rejareja, Andrew Lyimo
Wafanyakazi wa NBC Tawi la
Mbagala pamoja na maofisa wengine wa benki hiyo wakipozi kwa picha mbele ya
gari aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ atakalojishindia mmoja wa washindi sita wa
kampeni ya akaunti ya Malengo ya benki hiyo. Washindi wengine 24
watajindishindia pesa taslimu shs milioni moja kila mmoja.
Comments