Monday, June 24, 2013

RAIS KAGAME AFANYA MABADILIKO JESHINI

kagame 7f7aeRais Kagame afanya mabadiliko kwenye uongozi mkuu wa jeshi na kumteua Jenerali Patrick Nyamvumba kuwa mkuu mpya wa majeshi.

Jenerali Patrick Nyamvumba amechukua nafasi ya jenerali Charles Kayonga aliyeshikilia nafasi hiyo tangu mwaka 2002.
Mkuu mpya wa majeshi ya Rwanda,alikuwa kamanda wa kikosi cha umoja wa mataifa cha kulinda amani UNAMID katika jimbo la Darfur nchini Sudan tangu mwaka 2009.
Mabadiliko hayo pia yameshuhudia wadhifa mpya katika uongozi wa jeshi la Rwanda, ambao ni wadhifa wa mkaguzi mkuu wa jeshi uliopewa Brigedia jenerali Jack Nziza baada ya kupandishwa cheo na kuwa meja jenerali.Jack Nziza amekuwa akihudumu kama mkurugenzi mkuu katika wizara ya ulinzi.Pia mkuu wa zamani wa idara ya upelelezi wa nje kanali Dany Munyuza ameteuliwa kuwa naibu kamishna mkuu wa polisi ya Rwanda.Sababu za mabadiliko hayo hazijawekwa wazi. Chanzo: bbcswahili

No comments:

MSAJILI WA HAZINA AZINDUA MPANGO MKAKATI WA NMB 2026-2030

Mwandishi wa OMH Dar es Salaam. Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, amezindua Mpango Mkakati wa Muda wa Kati wa Benki ya NMB wa mwaka...