KATA YA THEMI WATAKA MAENDELEO KWANZA NA SI VURUGU


 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Themi na kuwaambia wasirudie kosa la kudharauliwa kwa kuchagua watu wasiotambua thamani ya kura zao.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahakikishia wana Themi kuwa wakati huu ni wa kuirudisha heshima ya Arusha na kwa kumchagua mgombea wa CCM kutasaidia sana kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika mji huo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimtambulisha mgombea wa kiti cha udiwani kata ya Themi, Victor G. Mkolwe, Juni, 13,2013 .
 Mgombea wa kiti cha udiwani kata ya Themi, Victor G. Mkolwe akihutubia wakazi wa kata hiyo na kuwaelezea moja ya mikakati yake ya kuleta maendeleo kwa wakazi hao,ambpo pia aliwaambia yeye hatangulizi siasa bali maendeleo na anatambua wakazi wake vizuri na changamoto zao na namna ya kuwasaidia.
 Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha, Catherine Magige akihutubia wakazi wa kata ya Themi ambapo pamoja na kuwaomba kumpigia kura mgombea wa udiwani kwa tiketi ya CCM pia aliahidi kuwasaidia wakina mama Wajane ambao walitelekezwa na ahadi za uongo za vyama upinzani.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya wakina mama Wajane ambao walidanganywa na vyama vya upinzani na sasa wamerejea CCM.
Wajane wa kata ya Themi wakisalimiana na mbunge wa viti maalum wa mkoa wa Arusha ,Catherine Magige. 
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na vijana wa Arusha mjini waliokuwa wakijiburudisha na mchezo wa karata.
 Meya wa Jiji la Arusha, Ndugu Gaudence Lyimo akihutubia wakazi wa kata ya Themi na kuwataka wasifanye makosa katika uchaguzi huu.
Rehema Mohamed maarufu kama Iron Lady akihutubia wakazi wa kata ya Themi ambapo aliwataka wakazi hao kuwa makini sana na wanasiasa wasiokuwa na mipango ya maendeleo.
 Kikundi cha ngoma cha Kambarage kikiburudisha wakazi wa kata ya Themi wakati wa mkutano wa kampeni za udiwani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi.
 Kijana anayefahamika kwa jina la Mboya ambaye alikuwa mstari wa mbele katika harakati za Chadema,akihutubia wakazi wa kata ya Themi wilaya ya Arusha mjini na kuwaambia wasirudie kuchagua vyama ambavyo kura yao itapotea kwa matapeli wa kimataifa.
 Nico ambaye naye alikuwa mstari wa mbele kuongoza mipango michafu ya kuvuruga amani ya Arusha, amekiri kuwa chama pekee cha kisiasa Tanzania kwa sasa ni CCM na ameomba wakazi wa kata ya Themi kuungana na kumchagua diwani anayetokana na CCM ili kuleta maendeleo na si migomo.
 MNEC wa wilaya ya Arusha mjini Godfrey Mwalusamba akihutubia wakazi wa kata ya Themi,ambapo aliwaambia kuna uhumu wa kufanyia kazi maendeleo yao zaidi kuliko kushabikia vitu visivyo na tija.

Comments