MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI KWENYE ENEO MAALUM LA UWEKEZAJI LA TANGA ECONOMIC CORRIDOR SEZ

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Viwanda, katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika jana Juni 21, 2013 jijini Tanga. Kushoto kwa Makamu ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tanga Economic Corridor Ltd, Chris Incheul Chae.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wakazi wa jijini Tanga, wakati alipofika eneo la Pongwe jijini Tanga jana Juni 21, 2013 kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Viwanda katika eneo hilo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, linalosimamiwa na Wawekezaji kutoka nchini Korea Kusini.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa ramani ya ujenzi wa Viwanda hivyo, mara baada ya uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Viwanda, katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika  jana Juni 21, 2013 jijini Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa baadhi ya vifaa kama Solar Cooker, ambavyo ni baadhi ya vitakavyokuwa vikizalishwa katika Viwanda hivyo baada ya kukamilika, mara baada ya uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Viwanda, katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika jana Juni 21, 2013 jijini Tanga
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda Mti wa kumbukumbu katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, baada ya kuweka rasmi Jiwe la Msingi la ujenzi wa viwanda katika eneo hilo wakati wa sherehe hizo zilizofanyika jana Juni 21, 2013 jijini Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa, Mwenyekiti wa Bodi ya Tanga Economic Corridor Ltd, Chris Incheul Chae na viongozi wengine kwa pamoja wakifurahia baada ya Makamu kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Viwanda, katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika jana Juni 21, 2013 jijini Tanga
 Makamu wa Rais na baadhi ya Viongozi, wakishirikiana kurusha mchanga ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa ujenzi wa viwanda hivyo.

 Picha ya pamoja.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Comments