Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA)imeitaka Star Tv irudishwe kwenye Star Times kabla ya saa kumi jioni leo.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof John Nkoma.
--
TCRA imeagiza Chaneli ya Star Tv irudishwe mara moja kwenye Star Times kabla ya saa kumi jioni leo.

Aidha Star Times na Star TV wameelezwa kuwa wote wamevunja sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya 2010 na Kanuni zake na kutakuwa kujitetea tarehe 17 Juni 2013.
Agizo la kurudishwa kwa Chaneli ya Star TV linatakiwa kutekelezwa ili kuhakikisha kuwa wananchi hawanyimwi haki ya kupata habari.

Vile vile wote wametakiwa kufuata Sheria inapotokea kutokuafikiana badala ya kutoa maamuzi bila kumshirikisha Mdhibiti (TCRA).

Comments