
Ilikuwa ni simanzi kwawale hasa
waliokuwa wakipata Burudani kutoka kwa Albert Mangwair na hakika
aliyethibitisha kwa kuona kuwa sasa amelala na hainuki hadi Masiha
atakapo rudi walishindwa kujizuia kwa vilio kama Rasta huyu kutoka
Ukonga Mazizini maarufu kwajina la Simaga akitokwa na machozi baada ya
kutoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Albert Mangwea katika
viwanja vya Lidaz Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mamia ya Wakazi wa jiji walijitokeza
kumuaga Msanii huyo wa muziki wa kizazi kipya aliyefariki Mei 28, mwaka
huu Nchini Afrika Kusini alikokuwa kwa shughuli za kimuziki.
Mangwewa alisafirishwa mchana wa ljana kwenda Kihonda mkoani Morogoro kwa mazishi yatakayo fanyika leo.

Wasanii wa Bongo Movie wakipita kutoa heshima za mwisho kwa Mwili wa marehemu.

Wasananii wa muziki nao wakipita kutoa heshima za mwisho.

Hata wanahabari nao kama Issa Mnali walitoa heshima za mwisho.

Ras Simaga akipita na zana zake baada ya kutoa heshima za mwisho.

Miraji Kikwete akizungumza machache na Ummy Wenselaus 'Dokii' viwanja vya Lidaz

Juu ni wana Dar es Salaam wakiwa katika folenina chini watu wachache waliokuwa wameketi.

Wanafamilia wakiwa katika jukwaa lao.

Wadau wakubwa wa kazi za Ngwair wakiwa katika pozi la majonzi.

Wakazi
wa jiji wakiwa na majonzi
Kamati ya Maandalizi ya Mazishi ya Ngwair ikiwa jukwaani.
No comments:
Post a Comment