Mwana
dada nguli katika Sanaa ya Muziki nchini Tanzania na Mshindi wa Tuzo ya
Mwanamuziki bora wa kike mara kadhaa na mwaka huu, Judith Wambura a.k.a
Lady JayDee a.k.a Jide a.k.a Mama somefood a.k.a Komando hatimaye usiku
wa kumakia jana alifanya show yake kali ya kutimiza miaka 13 katika
sanaa ya Muziki nchini.
Show
hiyo kali na ya aina yake ambayo awali ilikuwa ifanyike Mei 31, mwaka
huu katika ukumbi wa Nyumbani Lounge Kinondoni jijini Dar es Salaam
kufuatia kifo cha Msanii mwenzake Albert Mangwea ilifanyika jana licha
ya kuwa palitokea msiba wa msanii mwingine Langa.
Jide
ambaye alisindikizwa na wasanii kibao akiwepo Mkongwe Hamza Kalala,
Prof. J, Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye ni Mkongwe katika mziki wa Kizazi
kipya Joseph Mbilinyi 'Sugu', Juma Nature na wengine wengi.
Watu
wakiwa wamefurika kiasi cha kukosa kupenyeza mguu Lady JayDee
alitumbuiza jukwaani kwa nyimbo zake kadhaa za zamani ambazo zilionesha
kukonga vilivyo nyoyo za mashabiki na wapenzi wake ambao sasa
anawapeleka kwa staili ya Nyoka Mkali ANACONDA.
Sugu akiwa jukwaani
Sir Juma Nature akimtambulisha M to the P ambaye nae alikuwepo ukumbini hapo.
Hii ndio Wanaumeeeee....!!!
Mambo ya Anaconda haya ...yalikuwepo live.
Mashabiki wakifuatilia show hiyo...
Hii ni burudani kwa staili ya Anaconda...
Christina Manongi 'Sinta' akifurahia burudani kali katika onesho hilo la Lady JayDee.
Lady JayDee akitumbuiza katika show hiyo..
Meneja wa Lady JayDee ambaye pia ni Mumewe Gadna Habash (kulia) akiwa na wasanii wa Bongo Movie.
Jay Dee akikusanya fedha alizotunzwa na mashabiki wake na kumkabidhi mama yake.
Lady Jay Dee akiwa katika pozi na mama yake mzazi.
Video ya show hiyo.
Lady JayDee akiimba na Prof. J kibao chake cha Joto Hasira
Judith Wambura akiimba na Mkongwe Hamza Kalala
Prof J akikamua jukwaani sambamba na DJ Choka
Hii ndo Anaconda Stile
Mziki
sio filamu kuwa mtu utakaa kitini na kuangalia bali mziki ni kucheza na
hasa pale mashairi na midundo vinapo kukuna....Pichani ni Mashabiki wa
burudani wakicheza show hiyo. Joyce Kiria na Salma Msangi Kimora
wanayarudi vilivyo.
Hii ndio Team Anaconda ikiwa katika uzi wao makini
Hivi
ndivyo hali ilivyo ndani ya Ukumbi huu wa Nyumbani Lounge,Namanga jijini
Dar es Salaam ambapo leo hii kuna bonge moja la show la Mwanadada
mkongwe kwenye tasnia ya muziki hapa nchini,Lady Jay Dee ambaye
anatimiza miaka 13 tangu alipoanza kazi yake ya muziki.katika show hii
wanamuziki mbali mbali watapanda jukwaani aliwepo Mh. Mbunge wa Jimbo la
Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu.
Wadau
mbali mbali wa muziki hapa nchini wapo ndani ya ukumbi huu hivi sasa
kusuhudia show hii ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa
muziki.
Ndani
ni nyomi la hatari,lakini nje nako watu bado wanataka kuingia huku
wengi wao wakisema kuwa "hata kama hakuna siti,sie tuko radhi kusimama
ilimradi tumsapoti Dada yetu.
Getini mambo yako namna hii.
Foleni bado ni ndefu na watu bado wanazidi kuingia ukumbini hapa hivi sasa.
Burudani ya Utangulizi ikiendelea.
Comments