Friday, June 14, 2013

MSANI MWINGINE MAHIRI WA HIP HOP TANZANIA AFARIKI DUNIA


Msaanii wa Muziki wa Kizazi Kipya ambaye ni chimbuko la Coca-Cola Pop Star mwaka 2004, Langa Kileo (28) amefariki dunia jana

Taarifa  zinaaarifu kuwa Langa amefikwa na umauti katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa Matibabu.

Chanzo cha taarifa hiyo kinaeleza kuwa Marehemu Langa alikuwa amelazwa hospitalini hapo kufuatia Malaria kali iliyomshika na kukimbizwa Hospitalini hapo kwa matibabu zaidi.

Langa alishiriki shindano la Pop Star akiwa na wenzake wengine wawili Sara Kaisi 'Shaa' na Witness Mwaijaga 'Witness' na waliunda kundi lilioenda kwa jina la Wakilisha.

Wakiwa na kundi la Wakilisha Marehemu langa na Wenzake hao walitamba sana kwa nyimbio mbili za 'Unaniacha Hoi' na 'Kiswanglish'.
Baadaye Sarah Kaisi (Shaa) alijitoa. Lakini Langa na Witness walifyatua kibao cha ‘No Chorus’. 

Baada ya hapo Langa alifyatua kibao chake cha kwanza akiwa mwanamuziki binafsi, ‘Matawi ya Juu’ ambacho Dj John Dilinga (JD) aliwahi kuelezea ni moja ya kazi nzuri kutoka kwake, licha ya dosari za matumizi ya lugha. 
 
Kibao chake hicho cha  'Matawi ya Juu' na video ya wimbo huo ikaingizwa katika mashindano ya MTV Base na baade kushinda tuzo ya Kisima nchini Kenya.

Aliwahi fanya kazi na wasanii mbalimbali wa nchini kama Fid Q na nje ya nchi kama vile kundi la Necessary Noise, Naaziz na Wyre (Kevin Wyre).

maisha ya Langa kimuziki yalianza kuporomoka pale alipoachia albam yake ya 'Langa' na kushindwa kuuza baada ya kukataliwa na wasambazaji na kuamua kujiingiza katika maisha ya uteja ya utumiaji wa madawa ya kelevya.

Baada ya jitihada za familia yake aliweza kuondoka katika maisha hayo ya uteja na alipo toka aliachia nyimbo za 'Bombokiata' na 'Mteja Aliyepata Nafuu'.

Langa alizaliwa mnano mwaka 1985 jijini Dar es Salaam akiwa tunda la wanandoa Vanessa Kimei na mumewe Mengisen Kileo.

Alipata elimu ya msingi katika shule ya Msingi Olympio na baade  Sekondari ya Loyola, zote za jijini Dar es Salaam.


Akiwa kidato cha pili alihamishiwa Kampala, Uganda katika Shule ya Vienna na baadaye Shule ya Hillside International Academy, huko huko Uganda. Baadaye alirejea nchini na kujiunga na masomo ya Stashahada ya Masoko katika Chuo cha Biashara Dar es Salaam (CBE), Kampasi ya Dodoma.

No comments: