Waziri Membe Akutana kwa Mazungumzo na Ujumbe wa Chama cha Ukombozi wa Palestina (PLO)


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akisisistiza jambo wakati alipokutana kwa mazungumzo na Mhe. Yaseer Khalid, Mjumbe wa Kamati Tendaji na Naibu Mwenyekiti wa  Chama cha Ukombozi wa Palestina  (PLO) walipomtembelea Wizarani  na Ujumbe wake tarehe 14 Juni, 2013. Mhe. khalid na Ujumbe wake wapo  nchini kwa mwaliko wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
 Mhe. Membe akimsikiliza Mhe. Khalid wakati wa mazungumzo yao.
 Mhe. Membe akipata maelezo kutoka kwa Bw. Abdallah Mtibora, Afisa Mambo ya Nje katika Kitengo cha Sheria wakati wa kusaini mkataba huo huku Balozi Abujais akimwelekeza Mhe. Khalid.
 Mhe. Membe na Mhe. Khalid wakisaini Mkataba wa Ushirikiano katika masuala ya michezo kati ya Tanzania na Palestina.
 Mhe. Membe na Mhe. Khalid wakionesha Mkataba huo mara baada ya kusaini.
 Wajumbe waliofuatana na Mhe. Khalid wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani). Kutoka kushoto ni Mhe. Dkt. Nasri Abujais, Balozi wa Palestina hapa nchini, Mhe. Bi. Jehad Abu Znead, Mjumbe wa Kamati Tendaji ya PLO na Mhe. Saleh Rafat, Mjumbe wa Kamati Tendaji ya PLO.
 Ujumbe kutoka Makao ya CCM uliofuatana na Mhe. Migiro
  Katibu wa CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro ambaye alifuatana na Ujumbe huo wa Palestina hapa Wizarani akimsikiliza Mhe. Khalid (hayupo pichani). Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya (katikati) na Bw. Seif Kamtunda, Afisa Mambo ya Nje wakifuatialia mazungumzo hayo.

 Picha zaidi wakati wa mazungumzo hayo.
Picha ya pamoja.Picha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Comments