KAMPUNI YA STEPS YANOGESHA TUZO ZA BONGO MOVIE

Photo: Mjumbe wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete kushoto akimkabidhi tuzo Haji Adamu kwa niaba ya Jimmy Mponda aliyeshinda msanii bora wa Filamu za Mapigano wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya kwanza nchini na kuandalia na kampuni ya Steps Picha na www.burudan.blogspot.com
Mjumbe wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete kushoto akimkabidhi tuzo Haji Adamu kwa niaba ya Jimmy Mponda aliyeshinda msanii bora wa Filamu za Mapigano wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya kwanza nchini na kuandalia na kampuni ya Steps Picha na www.burudan.blogspot.com
Mjumbe wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete wa tatu kushoto akiwapongeza baadhi ya wasanii wa marehemu Kanumba baada ya kuwakabidhi tuzo

Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps Dilesh Solanki akimkabizi tuzo ya mwongozaji bora wa filamu nchini kwa mwaka 2012 Vicent Kigosi ‘Ray ‘ wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo na kuhudhuriwa na wasanii wengi nchini hii ni kwa mara ya kwanza Steps inaandaa tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps Dilesh Solanki akifafanua jambo baada ya kumkabidhi tuzo Vicent Kigos ‘Ray’ ya mwogozaji bora wa filamu nchini kwa mwaka 2012 wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo na kuhudhuriwa na wasanii wengi nchini hii ni kwa mara ya kwanza Steps inaandaa tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Steps wakipokea tuzo

Baadhi ya wasanii wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa tuzo zao za kwanza kwa mwaka 2012 zilizodhaminiwa na kampuni ya Steps.
…………………………………………………………………………
KAMPUNI ya Usambazaji wa filamu ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita ilitoa tuzo kwa wasanii bora waliofanya vizuri katika tasnia ya filamu nchini kwa mwaka 2012 ikiwa ni kwa mara ya kwanza kuanzishwa kwa tuzo hizo
Akizungumzia tuzo hizo Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Direshi Solanki amesema kuwa tuzo hizo watakuwa wakizitoa kila mwaka kwa kuleta maendeleo ya filamu nchini kampuni hiyo iliyojikita katika kusambaza filamu za wasanii wameweka historia ya kuigwa kutokana na kuanzisha tuzo hizo
Baadhi ya washindi ambao walipatikana katika tuzo hizo wa kwanza ni Stevin Mangendela ‘Steve Nyerere’, Issa Mussa ‘Cloud 112′ Mohamed Nurdini ‘Chek budi’ Nice Mohamed ‘Mtunisi’ Iren Paul akinyakuwa msanii bora chipkizi wa kike
Wakati katika kinyanganyiro cha kumpata msanii bora wa kiume alinyakuwa Jacob Steven ‘JB’ huku msanii bora wa kike ikienda kwa mwana dada Irene Uwoya
na msanii bora wa filamu za mapingano ilikwenda moja kwa moja kwa Jimmy Mponda ‘Jimmy Masta’
Wakati katika kipengere cha muhongozaji bora wa filamu kilikwenda kwa vicent Kigosi’ Ray’ na kampuni yake ya RJ Filamu
mbali na hivyo kulikuwa na tuzo za heshima kwa wasanii waliofanya vizuri rakini kwa sasa awapo duniani moja ni kwa Stevin Kanumba,Saidi Kilowoko ‘Sajuki’ John Stefano,Hussein Ramadhani Mkiety,’Sharo Milionea’
Katika utoaji wa tuzo huzo kulikua na burudani nyingi zikiongozwa na Odama Bendi

Comments