Thursday, April 04, 2013

Mmiliki wa Ghorofa Liloporomoka Jijini Dar es Salaam na Wengine 11 Wapandishwa Kizimbani Jijini Dara es Salaam Wakikabiliwa na Mashtaka 24 ya Kuua Bila ya Kukusudia

 Mtuhumiwa namba moja wa mashitaka 24 ya kuua bila kukusudia Raza Hussein Ladha (kushoto) akiwa chini ya ulinzi wakati alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam pamoja na watuhumiwa wenzake kumi.
 Mtuhumiwa namba moja wa mashtaka 24 ya kuua bila kukusudia, Raza Hussein Ladha (kushoto) akipelekwa chini ya ulinzi wa polisi kuingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam jana.
Mtuhumiwa namba moja wa mashitaka 24 ya kuua bila kukusudia Raza Hussein Ladha (kulia) na watuhumiwa wenzake kumi wakisubiri kupandishwa kizimbani, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaa
Mtuhumiwa namba moja wa mashitaka 24 ya kuua bila kukusudia Raza Hussein Ladha (aliyevaa kanzu nyuma) akiwa na watuhumiwa wenzake mara baada ya kupandishwa kizimbani na watuhumiwa wenzake kumi, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.Picha na Francis Dande na Michael Jamson 
---
Mfanyabiashara Radha Hussein Ladha wa jijini Dar es Salaam, Diwani katika Manispaa ya Kinondoni, Ibrahim Mohamed maarufu kama Kisoki (59) na wenzao 9, jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 24 ya kuua bila ya kukusudia.

Katika kundi hilo pia wamo vigogo wa Manispaa ya Ilala ambao ni Mhandisi Mkuu, Mhandisi Charles Salu (48), Mhandisi wa Majengo Godluck Sylivester (35) Mbaga na Mkurugenzi Mkuu wa Mkaguzi wa Majengo, Willibrod Wilbard (42).

Washtakiwa wengine ni Mhandisi Mohamed Swaburi (61), Mhandisi Mshauri, Zonazea Oushoudada (60), Mkadiriaji Majenzi, Vedasto Nziko (59), Msanifu Majengo, Michael Hema (59), Msajili Msaidizi AQRB, Albert Mnuo na Ofisa Mkuu Mtekelezaji OQRB, Joseph Ringo.

Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi, Devotha Kisoka, Wakili wa Serikali, Tumain Kweka akisaidiana na mawakili wenzake watano, alidai kuwa washtakiwa walifanya makosa kinyume na kifungu cha 195 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho 2002.

Kweka anasadiana na wenzake Benard Kongora, Ladslaus Komanya, Neema Haule, Joseph Maugo na Mutalemwa Kishenyi.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao kwa pamoja Machi 29, mwaka huu katika Mtaa wa Indira Gandhi, Wilaya ya Ilala waliwaua bila ya kukusudia Yusuph Mohamed, Kulwa Khalfan na Hamada Mussa.

Mbali na watu hao, pia wanadaiwa kuwaua bila ya kukusudia Kessy Manjapa, Khamis Mkomwa, Boniface Benard, Suhail Ally, Salmani Akbar, Seleman Haji, Seleman Mtego, Sikudhani Mohamed, Ahmed Milambo, Salum Mapunda, Suleiman Rashid na John Majewa.

Wengine ni Mussa Mnyamani, David Severin Herman, William Joackim, Abdulrahman Mwiha, Emmanuel Christian, Mmanyi Ngadula, Adivai Desiki, Emmanuel Greyson na Augustino Kasiri.


Washtakiwa wote hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mashtaka yanayowakabili Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza hadi Mahakama Kuu.

Mawakili wa utetezi wakiongozwa na Wakili wa Kujitegemea, Jerome Msemwa waliiomba mahakama kutoa dhamana kwa wateja wao kwa sababu mashtaka ya kuua bila ya kukusudia yanayowakabili yanadhaminika.Kwa Habari zaidi bofya na Endelea...>>>>>

No comments: