Jamal Sambeke mtoto wa marehemu
akifunga jeneza la baba yake mara baada ya watu mbalimbali kutoa heshima
zao za mwisho nyumbani kwake njiro Themi Mkoani Arusha
Waombolezaji wakibeba jeneza la Bilionea Babu na kuweka kwenye gari maalumu tayari kwa
Watu wakitoa heshima za mwisho
Watoto wa marehemu Sia na Getrude waliovalia nguo nyeupe
Jamal akifunga jeneza la marehemu Babu Sambeke
Jaji Aisha nyerere msibani pamoja na mkurugenzi wa kibo palace Vicent Laswai
Baadhi ya magari ya kifahari yaliyofika katika msiba huo
Mkurugenzi wa hoteli ya Kibo Palace Vicent Laswai akizungumza msibani mara baada ya watu mbalimbali kutoa heshima zao za mwisho
Waombolezaji
Mamia ya vigogo pamoja na watu
mbalimbali wafurika nyumbabi kwa marehemu Bilionea “Babu Sambeke”Ernest
Sambeke eneo la njiro jijini Arusha kuaga mwili wake unaotarajiwa
kuzikwa kesho nyumbani kwake eneo la Karanga mjini Moshi huku msiba huo
ukiwa tofauti na misiba mingine iliyozoekeaka hapa Nchini
Marehemu,Sambeke alifariki
hivi karibuni katika ajali ya ndege aliyokuwa akiiendesha na pia
mmiliki wa ndege hiyo ambapo ilianguka katika eneo la Kisongo na
kusababisha kifo chake Mkoani Arusha
Shughuli za kuaga mwili wa
marehu zilikamilika majira ya saa 8:45 mchana huku mwili huo ukipakiwa
katika gari maalumu la kifahari tayari kusafirishwa kuelekea nyumbani
kwake Moshi kwaaajili ya mazishi
Taratibu za kuaga mwili wa
marehemu zilianza majira ya saa 5 asubuhi huku wafanyabiashara wa
madini pamoja wafanyabiashara wengine kutoka hapa Arusha na Moshi
walionekana kutawala msiba huo
.
Katika zoezi hilo la kuaga
mwili wa mareheu Padri Florentine Mallya ambaye ni mdogo wa marehemu
aliongoza misa ya kumuombea marehemu na baada ya kumaliza alitoa fursa
kwa watu mbalimbali kupita mbele ya jeneza kwaajili ya kuaga mwili
Ndani ya jeneza marehemu
alivalishwa nguo zake za kirubani huku ,baadhi ya wanajeshi kutoka jeshi
la Wananchi Tanzania (JWTZ) walionekana jana katika zoezi la kuuaga
mwili wa marehemu ambapo baadhi yao walikuwa wamevalia sare za jeshi
hilo
Hatahivyo,baadhi ya watu walionekana katika hali ya kawaida huku watoto wakionekana na nyuso za huzuni mda wote
Tofauti na misiba mingine nchini
watu mbalimbali walipata fursa ya kupata chakula na vinywaji
mbalimbali kwa kujihudumia vikiwemo vinywaji aina ya Bavaria ambapo watu
waliohudhuria zoezi hilo walionekana wakijihudumia zaidi vinywaji vya
bavaria
Magari ya kifahari yalionekana
kutawala msiba huo huku barabara ya njiro ikionekana kuwa na msongamano
kubwa iliyosababishwa na zoezi hilo la uwagaji wa mwili
Marehemu aliacha watoto watatu ambao ni Sia,Jamal,Getruda
Comments