Mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana yatia Fora Mkoani Morogoro

 Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana ukionzwa na waendesha pikipiki baada ya kuwasili mjini Morogoro leo Aprili 14, 2013, Kinana anaaza jana ziara ya kikazi mkoani humo.
Baadhi ya waendesha pikipiki wakionekana kuwa na hamasa kubwa wakati wakisindikiza msafara wa Kinana kuingia mjini Morogoro  jana
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro, Innocent Edward, wakati wa mapokezi yake yaliyofanyika eneo la Nane Nane, nje kidogo ya mji wa Morogoro,jana. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Morogoro mjini Fikiri Juma. Kinana amewasili mkoani Morogoro kwa ajili ya ziara ya siku nane kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa ilani ya CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi baada ya kuwasili eneo la Nane Nane mkoani Morogoro kuanza ziara ya siku nane ya kikazi mkoani humo,jana Aprili 14, 2013.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi baada ya kuwasili Ofisi Kuu ya CCM mkoa wa Morogoro,jana Aprili 14, 2013. Kinana amewasili Morogoro kwa akili ya kukagua uhai wa Chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akijaribu kuwasha boda boda baada ya kuwasili Ofisi Kuu ya CCM mkoa wa Morogoro,jana Aprili 14, 2013.Yumo kwenye Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aliyewasili Morogoro kwa akili ya kukagua uhai wa Chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama.

Comments

Anonymous said…
I read this post completely on the topic of
the comparison of newest and preceding technologies, it's remarkable article.

Also visit my blog post - Reisen in die Türkei