Waziri Dk Fenella Mukangara Akutana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Dianna Melrose

 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akiongea jambo na Balozi wa Uingereza nchini Dianna Melrose mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina yao yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Balozi huyo aliahidi kuendelea  kushirikiana na wizara hiyo katika sekta ya Vijana, Utamaduni, Michezo na  kuendelea kutoa mafunzo kwa maafisa habari wa Serikali na Taasisi zake.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akisalimiana  na Joseph Paync  ambaye ni afisa miradi kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini  alipomtembelea ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Uingereza nchini Dianna Melrose. 
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akibadilishana kadi ya mawasiliano (Business Card) na Balozi wa Uingereza nchini Dianna Melrose alipomtembelea ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam. Ubalozi wa Uingereza umeahidi  kushirikiana na wizara hiyo katika sekta ya Vijana, Utamaduni, Michezo na  kuendelea kutoa mafunzo kwa maafisa habari wa Serikali na Taasisi zake.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akimshukuru  Balozi wa Uingereza nchini Dianna Melrose kutokana na ubalozi huo kutoa mafunzo ya mitandao ya kijamii (Social Media)  kwa maafisa Habari wa Serikali na Taasisi zake yaliyofanyika mwezi wa tatu mwaka huu. Balozi huyo alimtembelea waziri Dk. Mukangara ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumsalimia na kuimarisha mahusiano baina ya  Wizara hiyo na Uingereza. 
Balozi wa Uingereza nchini Dianna Melrose (kulia) akimweleza Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara jinsi nchi yake itakavyoendelea kushirikiana na wizara hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa maafisa Habari wa Serikali na Taasisi zake.Picha na Anna Nkinda – Maelezo

Comments