Mkutano Mkubwa Wa Hadhara Uliyofanywa na Wabunge Wa Chadema Waliyosimamishwa Kuhudhuria Vikao Vitano vya Bunge na Naibu Spika Job Ndugai
Mbunge wa Ilemela-Chadema Highness Kiwia akiunguruma mbele ya Maelfu ya Wanachama wa Chadema Mkoani Mwanza
Mbunge wa Iringa-Mjini-Chadema Mchungaji Peter Msigwa
Sehemu
ya Maelfu ya Wanachama wa Chadema Mkoani Mwanza Wakiwasikiliza Mbunge
wa Iringa-Mjini-Chadema Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa
Ilemela-Chadema Highness Kiwiawalipokua wakihutubia mkutano wa Hadhara
Mwanza Jana.Picha na Chadema
--
Wabunge sita wa Chadema waliosimamishwa bungeni wameamua kwenda
kuwashtaki Spika Anne Makinda na Naibu wake Job Ndugai kwenye majimbo
yao.
Wakitangaza uamuzi huo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi ya Mbugani, Mwanza jana, walisema pia watakwenda kwenye majimbo ya wabunge wawili wa CCM, Mwigulu Nchemba (Iramba Magharibi) na Livingstone Lusinde (Mtera) ili kueleza jinsi wabunge wa upinzani wanavyokandamizwa bungeni.
Ndugai, ambaye ni Mbunge wa Kongwa (CCM),
aliwasimamisha wabunge sita wa Chadema kuhudhuria vikao vitano vya Bunge
kutokana na kile alichokiita kufanya vurugu bungeni. Hatua hiyo ya
Ndugai aliyoichukua Aprili 17, mwaka huu ilipata baraka za Spika Makinda
Ijumaa iliyopita.
Wabunge waliosimamishwa ni Tundu Lissu (Singida
Mashariki), Godbless Lema (Arusha Mjini), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Mbeya
Mjini), Highness Kiwia (Ilemela), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini)
na Ezekiah Wenje (Nyamagana). Katika mkutano huo ulioanza saa 9.30
alasiri na kumalizika saa 12.00 jioni, ulihudhuriwa na wabunge wanne
kati ya hao. Mbilinyi ndiye aliyekuwa wa kwanza kuhutubia akifuatiwa
Mchungaji Msigwa, Kiwia na Wenje. Lissu na Lema hawakuhudhuria.
Akizungumzia ziara yao katika majimbo ya viongozi
hao wa Bunge, Mchungaji Msigwa alisema itakuwa ya kuwashtaki kwa
kuendesha Bunge kuwapendelea wabunge wa CCM hata wanapofanya makosa ya
wazi.Kwa Habari Zaidi Bofya na Endelea.......>>>
Comments