Monday, April 01, 2013

PROFESA JAY NA FID Q WAFUNIKA ILE MBAYA KATIKA TAMASHA LA VODACOM COCO BEACH

 
 Msanii wa kizazi kipya wa muziki wa Hip Pop nchini Dar Stamina akiwapagawaisha mashabikiwaliofurikakatikaufukwewaCoCo BeachkatikaTamasha la wazi la Vodacom Tanzania, lililofanyika katika Ufukwe wa huo, jijini Dar esSalaam,lilohudhuriwa na mashabiki lukuki, waliokwenda kujionea burudani hizo ambapo pia walitumia fursa hiyo kwa kuelimishwa kuhusu huduma na ofa mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo kama vile ChekaNaona Vodacom MAHELA.
Msanii mahiri wa mziki wa kizazi kipya Profesa Jay akiwapagawisha mashabiki waliofurika katika Tamasha la wazi la Vodacom, lililofanyika katika Ufukwe wa bahari ya hindi Coco Beach, jijini Dar esSalaam ,lilohudhuriwa na mashabiki lukuki waliokwenda kujionea burudani hizo ambapo pia walitumia fursa hiyo kwa kuelimishwa juu ya huduma mbalimbali zinazotelewa na mtandaowa Vodacom.
Msaniimahiriwa Hip Pop nchini Fid Q  a.k.a Ngosha akiingia katika steji wakati waTamasha la wazi la Vodacom Tanzania, lililofanyika katika Ufukwe wa Coco Beach, jijini Dar esSalaam,lilohudhuriwa na mashabiki lukuki, waliokwenda kujionea burudani hizo nakutumia fursa hiyo kwa kuelimishwa juu ya huduma mbalimbali zinazotelewa na mtandao wa Vodacom kama vile ChekaNaona Vodacom MAHELA.
  Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya  Fid Q akiandaa muziki katika kompyuta ya
kendogo(lap top) wakati wa Tamasha la wazi la Vodacom Tanzania, lililofanyika katika Ufukwe wa Coco Beach, jijini Dar es Salaam,lilohudhuriwa na mashabiki lukuki, waliokwenda kujionea burudani ambapo pia walitumia fursa hiyo kwa kuelimishwa juu ya huduma mbalimbali zinazotelewa na mtandao wa Vodacom,wanaoshuhudia kutoka kuliani Msanii machachari Dar Stamina  na AfisaUdhamini naMatukiawa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude.
Msanii wa Hip Pop nchini mzee wa michano Fid Q a.k.aakichana vilivyo wakati wa Tamasha la wazi la Vodacom Tanzania, lililofanyika katika Ufukwe wa Coco Beach, jijini Dar esSalaam,lilohudhuriwa na mashabiki lukuki, waliokwenda kujionea burudani hizo ambapo pia walitumia fursa hiyo kwa kuelimishwa juu ya huduma mbalimbali zinazotelewa na mtandao wa Vodacom kama vile ChekaNaona MAHELA inayofanya wateja wa kampuni hiyo kujishindia pesa taslimu.
Umati wa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya wa kipagawa na muziki wakati wa tamasha la Tamasha la wazi la Vodacom Tanzania, lililofanyika katika Ufukwe wa Coco Beach, jijini Dar esSalaam,lilohudhuriwa na mashabiki lukuki, waliokwenda kujionea burudani hizo ambapo pia walitumia fursa hiyo kwa kuelimishwa juu ya huduma mbalimbali zinazotelewa na mtandao wa Vodacom.
Baadhi ya mashabiki wa kifuatilia jinsi wanamuziki walivyokuwa wanachana katika Tamasha la wazi la Vodacom Tanzania, lililofanyika katika Ufukwe wa Coco Beach, jijini Dar esSalaam,lilohudhuriwa na mashabiki lukuki, waliokwenda kujionea burudani hizo ambapo pia walitumia fursa hiyo kwa kuelimishwa juu ya huduma mbalimbali zinazotelewa na mtandao wa huo kama vile Cheka NaonaVodacom MAHELA inayomfanya mteja wa kampuni hiyo kujishindia fedha taslimu.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Samsung wakiwa ayari kwa kutoa huduma mbalimbali zilizokuwa zikipatikana ikiwemo na uuzaji wa simu za bei rahisi zaTsh70,000 na 100.000 ikiwa ni sehemu ya ofa yaTamasha la wazi la Vodacom Tanzania, lililofanyika katika Ufukwe wa Coco Beach, jijini Dar esSalaam,lilohudhuriwa na mashabiki lukuki, waliokwenda kujionea burudani hizo ambapo pia walitumia fursa hiyo kwa kuelimishwa juu ya huduma mbalimbali zinazotelewa na mtandao wa huo.
 Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya nchini Joseph  Haule maarufu kama Profesa Jay akipanda jukwani tayari kwa kukonga nyoyo za mashabiki wake kwenyeTamasha la wazi la Vodacom Tanzania, lililofanyika katika Ufukwe wa Coco Beach, jijini Dar esSalaam, mahususi kwa ajili ya wateja wa kampuni hiyo,lilohudhuriwa na mashabiki lukuki, waliokwenda kujionea burudani hizo ambapo pia walitumia fursa hiyo kwa kuelimishwa juu ya huduma mbalimbali zinazotelewa na mtandao wa huo kama vile ChekaNaonaVodacom MAHELA.
----
Na Mwandishi wetu.
MKALI wamuziki wa Hip Hop nchini, Joseph Haule, maarufu kama Profesa Jay, juzi alifanya makubwa katika tamasha la wazi lililoandaliwa na Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania nakufanyika katika Ufukwe wa Coco Beach.

Mbali na Jay, wengine waliokuwapo na kufanya makubwa katika tamasha hilo lililohudhuriwa na watu wengi, alikuwapo Dar Stamina na Fid Q, ambapo wote kwa pamoja walifanikiwa kuwapatia burudani za aina yake.

Tamasha hilo lililofanyika maalum katika Sikukuu ya Pasaka, liliandaliwa maalum kwa ajili ya kusherehekea na wateja wao, pamoja na kuelimishwa kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni ya hiyo, ikiwapo Cheka Nao na promosheni ya Mahela, inayowawezesha wateja kujishindia pesa taslimu.

Akizungumza katika tamasha hilo, AfisaUdhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude, aliwashukuru Watanzania kwenda kwa wingi katika tamasha hilo la bure na kushiriki pamoja katika tukio hilo la kiburudani.

Alisema kuwa katika tamasha hilo, wateja wao walikuwa wakipewa elimu jinsi mtandao wao unavyofanyakazi, ikiwapo kujulishwa kwa huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo kwa kupitia tukio hilo lililofurika watu wengi.

"Sisi kama Vodacom tunashukuru kuwa pamoja na mashabiki wa muziki katika tukio hili la wazi lililoandaliwa mahususi kwa ajili yao, huku tukiamini kuwa tutaendelea kuwa pamoja kwa huduma mbalimbali zinazotolewa.

"Tunawaahidi kufanya kazi kwa moyo, pamoja na kuendeleza promosheni zenye mguso wa aina yake, ikiwapo hii ya Vodacom Mahela, ambapo wateja wetu wanapata fursa ya kujishindia fedha taslimu kutoka kwetu," alisema Kaude.

Aidha, msanii Profesa Jay alikuwa wa kwanza kupanda jukwaani kuwapatia burudani mashabiki wake na kuungwa mkono, sambamba na kuwaimbisha kila wimbo aliotaka kuimba katika tamasha hilo lililokuwa na mvuto wa aina yake.

Baada ya kushuka kwa msanii huyo, alitoa fursa ya Stamina kupanda, huku dakika kumi baadaye, Fid Q naye alipanda na kufanya shoo pamoja na mkali huyo wa Hip Hop anayekubalika na watu wengi kutokana na nyimbo zake kali, ukiwapo wa 'Kabwela'.

Tamasha la wazi la Vodacom lililofanyika kwa siku mbili katika ufukwe huo wa Coco Beach, ambapo wateja wao wote walipata fursa ya kushuhudia burudani hiyo bila kutoa kiingilio cha aina yoyote.

No comments: