DR. SALIM AHMED SALIM AONGOZA MAADHIMISHO YA 19 YA MAUAJI YA KIMBARI YALIYOTOKEA NCHINI RWANDA YALIYOFANYIKA DAR
Maandamano ya raia wa
Rwanda wanaoishi nchini Tanzania pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali
za jijini Dar es Salaam wakijipanga katika ukumbi wa New World Cinema
tayari kuanza maandamano ya kuadhimisha miaka 19 ya mauaji ya Kimbari ya
Rwanda kuelekea ukumbi wa mikutano wa Mlimani City.
Picha juu na chini Umati wa maandamano yakielekea katika ukumbi huo.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Dr. Salim Ahmed Salim njiani kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano Mlimani City.
Mgeni rasmi Dr. Salim
Ahmed Salim (wa tatu kulia) akiwa na balozi wa Rwanda nchini Tanzania
Mh. Benjamin Ruganganzi (wa tatu kushoto) wakisubiri kupokea maandamo ya
maadhimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda katika viwanja
vya Mlimani City jijini Dar.
Dr. Salim Ahmed Salim akipokea rasmi maandamano hayo.
Mgeni rasmi katika
maadhimisho ya 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda Dr. Salim Ahmed Salim
akizungumzia kumbukumbu ya mauaji hayo ambapo amesema historia ipo kwa
ajili yetu sote kujikumbusha yaliyopita ili tuweze kupanga yajayo na
kuwa mauaji ya Kimbari ni mzigo wetu sote na tunapaswa kujifunza
kutambua alama za watu wa jamii moja kuanza kuhitilafiana na kutafuta
namna ya kuzitatua kabla hazijaleta athari.
Na pia alichukua fursa
hiyo na kunukuu maneno yaliyowahi kusemwa na Baba wa Taifa wa Tanzania
Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere " Ukweli ni kwamba kila sehemu ya
Afrika ina ihitaji Afrika kwa pamoja na Afrika kama bara inahitaji kila
sehemu ya bara la Afrika".
MC katika maadhimisho ya
miaka 19 ya mauaji ya Kimbari Usia Nkhoma akirekebisha kipaza sauti
wakati mgeni rasmi akizungumza wakati wa maashimisho hayo.
Wageni waalikwa
wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa kumbukumbu
ya maashimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari Rwanda.
Kaimu Mratibu Mkazi wa
Umoja wa Mataifa nchini Bw. Jama Gulaid ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi
wa UNICEF akizungumza wakati maadhimisho ya miaka 19 ya mauaji ya
Kimbari nchini Rwanda yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo katika
ukumbi wa mikutano wa Mlimani City ambapo amesema dunia nzima itakuwa na
siku maalum ya kukumbuka wahanga wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda kwa
heshima ambayo ni alama ya kukumbuka athari za mauaji hayo na kuwa
pamoja na walionusurika na kwa namna nyingine ni alama msingi ya
kupongeza hatua zilizochukuliwa na jamii ya Wanarwanda kuungana pamoja.
Katika mazungumzo yake
alinukuu maneno yaliyozungumzwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban
Ki Moon " Katika maasdhimisho ya 19 ya mauaji ya Rwanda tunawakumbuka
watu zaidi ya 800,000 wasio na hatia ambao walipoteza maisha yao na
tutanendelea kuwaheshimu walionusurika na tutaendelea kuwa nao pamoja na
kukemea wale wote waliohusika na tukio hilo, na kuwapongeza
waliojitokeza kuzuia mauaji hayo yasiendelee".
Balozi wa Rwanda nchini
Tanzania Mh. Benjamin Ruganganzi akitoa salamu zake kwa wageni waalikwa
pamoja na watu waliohudhuria maadhimisho ya 19 ya mauaji ya Kimbari ya
Rwanda na kuhakikisha kuwa wananchi wa Rwanda wataendelea kudumisha
uhusiano na ushirikiano pamoja na nchini zingine za Afrika Mashariki ili
kuhakikisha tukio kama hilo halitajirudia tena.
Sehemu ya wageni waalikwa wakiwemo mabalozi mbalimbali wakimsikiliza Balozi wa Rwanda nchini (hayupo pichani).
Msemaji wa Mahakama ya
Umoja wa Mataifa ya Mauaji ya Rwanda (ICTR) Bw. Roland Ammousouga
akitoa kauli yake wakati wa maadhimisho ya 19 ya mauaji ya Kimbari ya
Rwanda ambapo amesema kwa miaka 19 iliyopita watu wanaweza wakajisifu
kazi iliyofanywa na mahakama ya ICTR kwamba imetimiza kilio cha maelefu
ya waathirika na kuwa imesaidia katika kuleta upatanishi na kuijenga
upya Rwanda sambamba na kuhamasisha amani na ulinzi katika ukanda wa
Afrika wa maziwa makuu, wakati haikufanikiwa kuwakamata wale wote
waliohusisha na mauaji hayo kwa kutoa itumia Rwanda kuwatafuta wahusika 6
waiojulikana walipo ili waweze kukabiliana na kesi zinazowakabili
kinachojionyesha hapa ni kwamba ICTR inaashiria kwamba mapambano dhidi
ya mazingira ya wahusika wengine 3 hawawezi kukamatwa.
Umati wa watu waliofurika (chini) katika maadhimisho hayo wakiwemo wanafunzi wa shule ya sekondari Jitegemee (juu).
Mmoja wa viongozi wa Dini akiomba dua ya kuwarehemu walipoteza maisha katika mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda.
Meza kuu ikiongozwa na
mgeni rasmi Dr. Salim Ahmed Salim kuwasha mishumaa ikiwa ni ishara ya
kuwakumbuka watu waliopoteza maisha wakati wa mauji ya Kimbari nchini
Rwanda.
Comments