Wednesday, August 05, 2009

Waandishi wa habari waachiliiwa huru


Wenzetu Wamarekani wana raha saana yaani tukio la waandishi wa habari wawili kufuatwa na Rais Mstaafu, Bill Clinton lina maana kubwa ukiachia ukubwa wa tatizo lenyewe. Hivi kuna Watanzania wangapi huko nje ya nchi wanaotaabika kutokana na kushikwa kwa masuala ya msingi kabisa.
Rais huyo wa zamani wa Marekani, Clinton aliwasili jana Marekani akitokea Korea Kaskazini ambako alikwenda kusaidia waachiliwe huru.
Waandishi hao wawili wa habari, Laura Ling na Euna Lee, wamekuwa kuzuizini nchini Korea Kaskazini kwa zaidi ya wiki ishirini, na leo wamerejea nyumbani kwao Marekani na kupokelewa vyema na familia zao.

Bwana Clinton aliwasili nchini Korea Kaskazini hapo jana na kukutana na kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-Il.

Lengo la ziara yake ilikuwa ni kuhakikisha waandishi hao wawili wameachiliwa huru.

Waandishi hao walikuwa wamehukumiwa kifungo cha miaka kumi na mbili jela kwa kosa la kuingia nchini Korea Kaskazini kinyume cha sheria.

Bila shaka kuachiliwa huru kwa waandishi hao wa habari ni ushindi mkubwa katika uhusiano wa Marekani na Korea Kaskazini. Hata hivyo, bado ni mapema kusema kama hatua hii itasaidia katika kuleta diplomasia ya kudumu kati ya nchi hizi mbili.

Uhusiano kati ya Marekani na Korea Kaskazini umezorota chini ya Rais Barack Obama, huku Korea Kaskazini ikifanya majaribio yake ya zana za kinuklia.

Wengi wanachukulia hatua ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini kama jaribio la kutaka kuheshimiwa na jamii ya kimatiafa.

Ingawa ziara ya Bill Clinton ilisemekana kuwa ya kibinafsi, Bwana Clinton angeweza kuchunguza hali ya kiafya ya Kim Jong-Il, hali yake ya kiakili na kama kuna uwezekano wa kuanzisha upya diplomasia na Marekani.

Hata hivyo, Bill Clinton anaelewa vyema kuwa ni vigumu kutabiri taabia ya Korea Kaskazini. taarifa zaidi http://news.yahoo.com/s/ap/us_nkorea_journalists_held

No comments: