Thursday, August 13, 2009

Ngugi wa Thiong'o alia kasi ya usomaji kushuka



MTUNZI gwiji wa vitabu barani Afrika, Profesa Ngugi wa Thiong'o amesema idadi ya Waafrika wanaosoma vitabu imeshuka na kutishia maendeleo ya watu barani kutokana na kutegemea kazi za waandishi wa nchi za Magharibi.

Ngugi alisema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa Kongamano la Sita la Usomaji kwa Wote linalofanyika Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa siku tano kuanzia jana.

Alisema tatizo hilo linasababishwa na nchi zinazoendelea kutegemea sana misaada kutoka nchi tajiri na hivyo wananchi wake kujikuta wakitegemea vitabu kutoka nje ambavyo vinapotosha badala ya kazi za waandishi wa barani Afrika.

Ngugi, mtunzi wa kitabu cha fasihi cha "Decolonising the Mind (kuondoa ukoloni wa akili)", alisema kuendelea kufanya hivyo ni kuendeleza ukoloni Mamboleo ambao alisema maendeleo hupimwa kwa kuangalia idadi ya walionacho badala ya kuangalia watu wa kipato cha chini.

“Maendeleo ya Afrika sio ya kutegemewa kwa sasa kwa kuwa sera za nchi zetu zinalenga kuwafurahisha watu wa nchi za magharibi kwa kuwa ukoloni mamboleo bado upo; utake,a usitake,” alisema mwanafasihi huyo mkongwe kutoka Kenya. Habari ya Aziza Athuman na Neema Rugemalira wa Mwananchi

1 comment:

SEDOUF said...

HONGERA BWANA NGUNGI.

RAIS DKT. SAMIA AKUTANA NA UJUMBE WA JUKWAA LA MABUNGE LA NCHI ZA MAZIWA MAKUU (FP-ICGLR) IKULU NDOGO TUNGUU, ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Kiongozi wa Jukwaa la Mabunge la...