KHARTOUM, Sudan
HUKUMU ya mwanamke mwandishi wa habari aliyekamatwa kwa madai ya kuvaa suruali iliyotarajiwa kutolewa jana nchini Sudan imeahirishwa , baada ya polisi kulzimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya mamia ya waandamanaji waliokuwa nje ya mahakama.
Jaji anayesikiliza kesi hiyo inayomkabili mwanamke huyo ambaye pia ni mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Lubna Ahmed al-Hussein, ambaye pia ana kinga ya UN ililazimika kuahirishwa hadi Septemba.
Lubna ambaye yupo katima umri wa zaidi ya miaka 30 alikamatwa wiki iliyopita pamoja na wanawake wengine 12 na kushtakiwa kwa kosa la kuvaa suruali, kinyume na matakwa ya sheria za kiislamu zinazotumika nchini humo, ambapo huenda akaadhibiwa kuchapwa hadi kufikia viboko 40.
Walifunguliwa mashitaka ya kutojiheshimu mbele ya jamii wakati akiwa katika mgahawa mjini Khartoum, na yeye alisema yuko tayari kushitakiwa na kuhukumiwa, hata kama ikibidi kuacha kazi UN.
“Niko tayari kujiuzulu UN, ninahitaji zaidi kesi hii iliyo mahakamani iendelee hadi mwisho wake,” alisema mara baada ya kufika mahakamani jana.
“Niko tayari lwa lolote litakalotokea. Kwa kweli siogopi kabisa kuhusu kesi hii. Iwapo nitahukumiwa kuchapwa viboko, au kwa namna nyingine nitakata rufaa. Nataka nione mwisho wake, hata katika mahakama ya kikatiba iwapo itawezekana,” aliongeza.
“Na iwapo mahakama ya Katiba itaeleza kuwa sheria ni Katiba, nipo tayari kuchapwa sio viboko 40 tu, lakini mara 40,000 zaidi,” alisema Lubna ambaye pia hufanya kazi katika gazeti la mlengo wa kushoto la Al-Sahafa.
Alieietiza kwua iwapo kuna watu wanaotumia sharia kama kigezo cha kuidhinisha unyanyasaji wa wanawake kwa sababu ya kile wanachovaa, anahitaji kuonyeshwa ni kifungu gani katika Quran au hadith (mafundisho ya mtume Mohammed) kinachoeleza hivyo, kwa kuwa hakuwahi kukiona.
Hatua hiyo imemfanya awe na mvutano na upande wa utetezi kutoka kwa wakili wake, baada ya wakili kumueleza Jaji kuwa Lubna ana kinga ya kutoshitakiwa na kumtaka Jaji asikubaliane na matakwa ya mwanamke huyo.
Comments