Wednesday, June 30, 2010

Muda wa usajili line waongezwa



SERIKALI imeongeza muda wa usajili wa simu za viganjani ili kuwezesha wananchi wengi waweze kujisajili baada ` kusikiliza kilio chao ili kuwapa fursa zaidi ya kujisajili.

Hayo yalisemwa jana Bungeni na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msollla wakati akiwasilisha hotuba yake ya makadrio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara hiyo.

“Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni sikivu imesikia kilio cha wananchi wengi. Imeongeza muda wa usajili wa simu za viganjani hadi Julai 15, mwaka huu baada ya hapo simu zote ambazo hazijasajiliwa zitafungwa,” alisema Profesa Msolla .

Aidha Waziri Msolla alisema jumla ya kampuni 14 hadi sasa zimepewa leseni ya kutoa huduma za mawasiliano ya simu.
Aliongeza kuwa idadi ya watumiaji wa simu kwa kigezo cha njia za simu (line) zinazotumika imefikia 18,207,390, hivyo idadi hiyo ni ongezeko la asilimia 400 ikilinganishwa na watumiaji 3,542,563 waliokuwepo mwaka 2005.

Alisema idadi ya simu za mezani hadi sasa ni 174,800 ilinganishwa na 154,420 zilizokuwepo mwaka 2005.

“Hii ni sawa na ongezeko la la asilimia 13.2 . ukuaji huu umepanua wigo wa mawasiliano ya simu na kuongeza huduma nyingine zinazoendana na matumizi ya simu hapa nchini

Alizitaja huduma hizo kuwa ni upatikanaji wa taarifa, huduma za mtandao, ulipaji wa Ankara za simu, maji, umeme na huduma za kibenki.

Awali Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitoa agizo kuwa namba zote za simu za mkononi zisajiliwe kati ya Julai 1, mwaka 2009 hadi Desemba 31, mwaka 2009.

Awali mamlaka hiyo iliongeza muda wa mara ya pili wa miezi sita wa kusajili simu hizo, kuanzia Januari mwaka 2010 hadi Juni mwaka huu baada ule wa kwanza kuonyesha watu wengi walikuwa hajajisajili. SOURCE: BUNGE.

Usajili wa line za simu mwisho leo


WATU wakiwa katika kibanda cha usajili wa namba za simu za mkononi. Zoezi hilo bado linaendelea Jijini Dar es Salaam. Picha na Amran Mnjagila.

*********************************************

Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema haitaongeza muda wa kusajili laini za simu za mkononi na kwamba namba yoyote ambayo itakuwa haijasajiliwa itafungiwa kupiga, kupokea simu pamoja na ujumbe wa maandishi (SMS).

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma alisema baada ya saa sita usiku ya Juni 30 namba yoyote ambayo itakuwa haijasajiliwa itafungwa kupiga, kupokea simu pamoja na ujumbe wa maandishi kwa siku 90 hadi Septemba 30 mwaka huu.

“Katika kipindi hiki cha siku 90 endapo mtumiaji atasajili namba yake itafungwa na kwa namba ambazo hazitakuwa zimesajiliwa ifikapo Septemba 30 zitafutwa na kuondolewa kwenye mitandao kabisa,” alisema Nkoma

Alisema Mamlaka hiyo imekubaliana na makampuni ya simu kufanya uhakiki wa usajiliwa laini za simu za wateja kwa kutumia namba 106 kupitia simu za mkononi na kwa wateja wa mitandao iliyoko katika mifumo ya GSM, wateja wanatakiwa kuingiza *106# , wateja wa mfumo wa CDMA watatakiwa kupiga namba hiyo na watapokea taarifa za usajili.

“Hivi karibuni muswada wa sheria ya mawasiliano ya kielektroniki na posta ulipitishwa na Bunge kwa sheria , sheria hiyo inafanya usajili wa namba za simu za mkononi kuwa ni wa lazima kwa mujibu wa sheria hiyo, kuanzia sasa na kutofanya hivyo ni kosa la jinai. Adhabu ni faini na kifungo au vyote kwa pamoja,” alisema Nkoma.

Mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka jana mamlaka hiyo ilitoa agizo kuwa namba zote za simu za mkononi zisajiliwe kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kuwalinda watumiaji dhidi ya matumizi mabaya ya huduma ya mawasiliano, kuwezesha na kurahisisha utambuzi wa wateja watumiao huduma mbalimbali, kuimarisha usalama wan chi na nk.

Wakizungumza mara baada ya tamko hilo la mkurugenzi wa TCRA, viongozi wa kampuni za simu za mikononi za TTCL, Zain, Tigo, Vodacom, Sasatel, BOL, kwa nyakati tofauti waliilalamikia hatua hiyo ya serikali wakisema kwamba iatawasababishia usumbufu wateja wao na kuwapa hasara kubwa.

Mkurugenzi Mkuu wa Zain Tanzania, Khaled Mehtadi alisema wanakubaliana na mpango huo wa serikali, lakini wanaomba uongezwe muda kwa kuwa kazi ya kukusanya data kutoka maeneo mbalimbali ya nchi ni kubwa na haiwezi kumalizika haraka kutokana na wateja wengi kujitokeza dakika za mwisho.

"Pia alisema kuwa iwapo serikali itaendelea kung'ang'ania uamuzi wake wa kufungia laini basi kampuni hiyo itapata hasara ya kadri ya asilimia 25 kwa kuwa wamewekeza fedha nyingi kulipa mawakala zaidi ya 50,000 nchi nzima na bado kazi haijamalizika,"alisema.

Kaimu Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya simu za mikononi ya TTCL, Ernest Nangi alisema kuwa kama walivyo waendeshaji wa kampuni zingine za simu wanaona kuwa bado wanahitaji muda kuweza kukabili changamoto hiyo.

Kwa upande wa kampuni za Tigo kupitia Meneja wa Huduma kwa Wateja, Harieth Rwakatare na Vodacom kupitia Mkurugenzi wake Francois Swart walisema kuwa zoezi hilo ni gumu na kwa maana hiyo wakaitaka serikali na wateja wao kuwa wavumilivu ili waweze kulikamilisha kama inavyopaswa. SOURCE: TCRA

Tuesday, June 29, 2010

Marubani wa JWTZ wafa ajalini



WANAJESHI wawili ambao ni marubani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wa Kambi ya Ngerengere mkoani hapa, wamekufa baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kuligonga gari la watalii na kupinduka.Ndege hiyo ya Jeshi ambayo inatumika katika mafunzo ya kijeshi, jana ilitua barabarani na kusababisha ajali iliyoua marubani wawili wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) baada ya kugongana na lori lililokuwa limebeba watalii.

Ndege hiyo ndogo yenye namba F59119 iligongana na gari hilo eneo maarufu kwa jina la Zimbabwe lililo Kijiji cha Manga, Kata ya Mkata wilayani Handeni.

Baadhi ya watu walioshuhudia ajali hiyo ya nadra sana kutokea walieleza kuwa waliiona ndege hiyo ikishuka kabla ya kutua katikati ya barabara na baadaye kujaribu kuruka tena, kitu kinachoonyesha kuwa rubani alikuwa katika harakati za kuinusuru.

Walisema, hata hivyo, ndege hiyo ilishindwa kuruka juu na kuserereka barabarani.
Walisema wakati ikiyumba, ndege hiyo nusura iligonge basi la kampuni ya Simba Mtoto lililokuwa likitokea jijini Tanga kuelekea Dodoma.

Kaimu kamanda wa polisi mkoani Tanga, Jafari Mohammedi ambaye alikuwa kwenye eneo la tukio hilo, aliwataja waliokufa kuwa ni rubani wa ndege hiyo Meja Kathbet Leguna (41) na mwanafunzi wake Luteni Andrew Yohana Kijangwa (31).

Mmoja wa wafanyakazi wa gari hiyo iliyogongana na ndege hiyo Solomon Talalai alisema ndani walikuwepo watu 24 ambao 19 kati yao ni raia kutoka Uholanzi, wanne kutoka Kenya na mmoja Mtanzania. Imeandikwa na Hussein Semdoe na Burhani Yakub, Handeni:SOURCE:MWANANCHI

Friday, June 25, 2010

Waziri Mkuu akutana na vijana wa Dodoma


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pmoja na Viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Dodoma baada ya kufungua kongamano la siku tatula Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Dodoma kwenye ukumbi wa African Dream Mjini Dodoma leo. (Picha na Ofisi ya Wazir Mkuu)

Thursday, June 24, 2010

Jaji Mkuu aapisha mawakili 128


Mke wa Rais Mama salma Kikwete, akimpongeza mwanae, Ridhiwani Kikwete, kwa kumpa shada la maua baada ya kutunukiwa Cheti cha kuwa Wakili wa kujitegemea, wakati wa hafla ya kuwatunuku mawakili 128, iliyofanyika kwenye viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam leo.






Jaji mkuu wa Tanzania Mh.Augustino Ramadhan leo amekabidhi hati za uwakili kwa mawakili 128 katika mahakama kuu jijini Dar es Salaam

Katika tukio hilo lililofanyika mapema leo tarehe 24 ambapo Mwenyekiti wa WAMA na mke mheshimiwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete amehudhuria na kushuhudia zoezi zima la kupatiwa kwa hati mawakili hao.

Aidha katika zoezi hilo limeonesha kuwa ni la kufurahisha kwa familia ya rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa mtoto wake ambaye sasa ni wakili Ridhiwani Jakaya Mrisho Kikwete kuwa miongoni mwa mawakili waliotunukiwa hati hizo leo.

Katika sherehe hizo pia mawakili wa kujitegemea walifika kushuhudia tukio hilo ambapo walifurahishwa sana na wenzano kutokana na uvumilivu waliokuwa nao hata kufikia hatua ya kupata hati ya kuwa Wakili.

Pia wamewataka mawakili hao kutumia vizuri heshima waliyopewa ili kuepukana na kinachoisumbua serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania(Utumiaji mbovu wa madaraka na kutokutenda haki)kitendo ambacho kinaitesa jamii nzima ya Watanzania.

Wednesday, June 23, 2010

Kinara wa mihadarati akamatwa Jamaica


Christopher Dudus jambazi sugu wa mihadarati Jamaica
Polisi nchini Jamaica wamemkamata kiongozi sugu wa biashara za mihadarati nchini humo Christopher Dudus Coke viungani mwa mji mkuu, Kingston.

Bwana Coke ambaye amekuwa akisakwa kwa muda mrefu, anatakiwa nchini Marekani kwa mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya pamoja na biashara haramu za silaha.

Juhudi za kumkamata Coke mwezi jana zilisabisha vurugu nchini humo ambapo watu zaidi ya sabini waliuawa.

Mkuu wa polisi nchini Jamaica, Owen Ellington, alisema kuwa maafisa wake wa polisi wameonywa dhidi ya kutokea vurugu zingine kufuatia kukamatwa kwa bwana Coke.

Huenda akafikishwa mahakamani katika muda wa masaa arobaini na nane.

Bwana Coke alitajwa kama mmoja wa majambazi sugu zaidi duniani, ingawa wafuasi wake wanasema yeye ni kiongozi wa jamii.

Ajitokeza kumvaa Dk Mwakyembe


Mratibu wa Kitaifa wa Shirika la Kazi Duniani(ILO) Rhoda Mwamunyange (mwenye blauzi ya pinki) akitangaza jana jijini Dar es salaam nia yake ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Kyela kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi. Jimbo hilo hivi sasa liko chini ya mheshimiwa Dkt Harrison Mwakyembe. Wengine kushoto ni Mpambe wa Rhoda na kulia ni Ofisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari Mwirabi Sise. Picha na Tiganya Vincent, Dar es salaam

RAIS SAMIA AKUTANA NA WAZEE WA MIKOA YOTE NCHINI, AFUNGUA UKURASA MPYA WA MAZUNGUMZO YA KITAIFA

  Dodoma, Agosti 27, 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na wazee wa Mkoa wa Dodoma pam...