Christopher Dudus jambazi sugu wa mihadarati Jamaica
Polisi nchini Jamaica wamemkamata kiongozi sugu wa biashara za mihadarati nchini humo Christopher Dudus Coke viungani mwa mji mkuu, Kingston.
Bwana Coke ambaye amekuwa akisakwa kwa muda mrefu, anatakiwa nchini Marekani kwa mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya pamoja na biashara haramu za silaha.
Juhudi za kumkamata Coke mwezi jana zilisabisha vurugu nchini humo ambapo watu zaidi ya sabini waliuawa.
Mkuu wa polisi nchini Jamaica, Owen Ellington, alisema kuwa maafisa wake wa polisi wameonywa dhidi ya kutokea vurugu zingine kufuatia kukamatwa kwa bwana Coke.
Huenda akafikishwa mahakamani katika muda wa masaa arobaini na nane.
Bwana Coke alitajwa kama mmoja wa majambazi sugu zaidi duniani, ingawa wafuasi wake wanasema yeye ni kiongozi wa jamii.
Comments