Friday, September 05, 2008

JK aongoza mazishi ya Mwanawasa


Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Rais Jakaya Kikwete akimfariji Patrick Mwanawasa mtoto wa kwanza wa kiume wa Rais wa Zambia Marehemu Dr.Levy Mwanawasa,wakati wa mazishi ya kiongozi huyo yaliyofanyika jijini Lusaka

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole Rais wa kwanza wa Zambia Dr.Keneth Kaunda wakati wa mazishi ya Rais wa Zambia Marehemu Dr.Levy Mwanawasa,yaliyofanyika jijini Lusaka Zambia jana.Rais Kikwete amerejea jijini Dar es Salaam jana jioni.
Mjane wa aliyekuwa Rais wa Zambia Maureen Mwanawasa akiwa katika majonzi wakati wa mazishi ya mumewe yaliyofanyika jana katika makaburi ya Embassy Park Lusaka Zambia

Wednesday, September 03, 2008

Sabato Masalia watimuliwa tena uwanja wa ndege


Polisi yatoa onyo la mwisho kwa Wasabato Masalia

KUNDI la waumini wa Dhehebu la Waadventista Wasabato Masalia, kwa mara ya tatu limesambaratishwa na askari wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, baada ya kurudi tena uwanjani hapo huku wakiwa wameongezeka idadi yao kutoka 17 hadi kufikia 51.

Wasabato hao masalia, walifika katika uwanja huo mnamo saa 2:00 asubuhi huku wakiwa na mabegi yao tayari kwa safari wakisema: "Bwana alikuwa amewaambia tena kuwa jana ilikuwa ndio siku ya kuondoka na kuelekea nchi za Ulaya kuhubiri injili."
Na Furaha Kijingo

Mzanzbari aliyamatwa na FBI kwa ugaidi arejeshwa



MTANZANIA aliyekamatwa namakachero wa Marekani kwa kuhusishwa na ugaidi, Suleiman Abdallah Salim (Morris), amerudishwa Zanzibar juzi na Shirika la Msalaba Mwekundu kutoka Afghanistan baada ya kubainika kwamba si gaidi.

Akizungumza na Mwananchi nyumbani kwao maeneo ya Mombasa, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar, huku akinekana mchovu, alisema alikamatwa na makachero wa FBI nchini Somali mwaka 2003 akiwa katika shughuli zake za kibiashara na kuingizwa katika gari bila ya kufahamu anapopelekwa.

Akielezea mkasa uliomkuta akiwa eneo la Abusasu, Mjini Mogadishu alisema baada ya kukamatwa na kuingizwa katika gari hilo huku akipata kipigo kutoka kwa maafisa
hao alisafirishwa hadi Nairobi, Kenya na kutakiwa apeleke mtu wa kudhamani, lakini aliwaambia kuwa yeye ni Mtanzania na hana kwamba ndugu yeyote jijini humo.

“Walinambia mimi ni Msomali nilikataa nikiwaambia kuwa ni Mtanzania. Kisha wakasema ni Myemen nikasema ni Mtanzania walipoona nasema kiswahili wakananimbia mlete ndugu yako akuwekee dhamana, nikawaambia sina jamaa Nairobi mimi
kwetu ni Tanzania,” alisimulia Salim.

Alisema baadae alirejeshwa tena Somali na kuwekwa kwenye kambi ya jeshi na kila mara alikuwa akiulizwa maswali huku akipata kipigo wakati akijibu maswali yao.

Alisema baadhi ya maswali aliyoulizwa yalihusu kama anawafahamu Khalfan, Marwan na Fahad na kutakiwa kusema hao ni akina
nani kwake na kwamaba aliwajibu kuwa anawafahamu kwa kuwa ni rafiki zake wa karibu aliokuwa akifanya nao kazi ya uvuvi maeneoo ya Mombasa kabla ya kwenda Somali. Habari ya Salma Said, Zanzibar.

Afya ya huyu jamaa itakuwaje baadaye


Kijana ambaye jina halikuweza kufahamika mara moja alikutwa akizibua choo bila ya kuwa na vifaa maalumu vya kujikinga na magonjwa ya milipuko hivi karibuni katika eneo la Manzese jijini Dar es Salaam. Picha ya Venance Nestory.

Tuesday, September 02, 2008

Mwana wa tanzania


Maisha ya Watoto wetu wa kitanzania kwa kiasi kikubwa yamegubikwa na mitihani mingi, na ili kuishinda inabidi kutumia jitihada kubwa hebu cheki mtoto huyu amejitwika mzigo wa kuni, hivi mustakabali wa mtoto huyu na wenzake ukoje iwapo baadhi ya wazee wetu wanaendelea kukoboa maliasili zetu zote kwa manufaa yao binafsi jamani tuisaidie Tanzania.

Sunday, August 31, 2008

Mtuhumiwa wa ujambazi akamatwa Dar akiwa amevaa baibui





Na Festo Polea

MTU mmoja ambaye anadaiwa kuwa jambazi maarufu amekamatwa jijini Dar es salaam likiwa amevaa vazi la Baibui ili asijulikane kiraisi akiwa amebeba shoka mgongoni kwa ajili ya kujihami.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Suleiman Kova, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mtuhumiwa huyo wa ujambazi alikamatwa juzi saa 1.30 usiku maeneo ya Kinyerezi Magengeni,jijini Dar es Salaam akiwa ajiandaa kufanya uhalifu.

Kova alisema mtuhumiwa huyo ni mkazi wa Kinyerezi Mwisho na kwamba alianza kufukuzwa baada ya jeshi la polisi kupokea taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuwa jambazi linalosakwa na polisi limeonekana katika eneo hilo likiwa limevaa baibui.

Alidai kuwa mtuhumiwa huyo akiwa katika mawindo yake juzi bila kujua kuwa anafuatiliwa, alipoona polisi alianza kukimbia na wananchi wakaanza kumfukuza k na kufanikiwa kumkamata na kuanza kumpa mkong’oto na polisi walifika na kumuokoa.

Kamanda Kova alifafanua kuwa wakati mtuhumiwa anakamatwa alikuwa amevaa baibui na kwamba isingekuwa rahisi kutambua kuwa ni mwanaume.

“Jambazi hilo licha ya kuvaa baibui pia lilikuwa limeficha shoka mgongoni ambayo huitumia kufanikisha mipango yake,” alisema Kova.

Aliongeza kuwa baada ya jambazi hilo kukamatwa ilibainika kuwa amewahi husika katika matukio mbalimbali ya unyang’anyi wa kutumia silaha jijini Dar es Salaam na mikoa ya jirani ya Morogoro na Pwani.

Katika hatua nyingine, wezi wanne ambao wanadaiwa kuiba magari, wamekamatwa jijini wakiwa katika harakati za kubadilisha namba za gari hayo mali.

Kamanda Kova alisema watuhumiwa hao walikamatwa juzi saa 10.30 jioni kwenye baa ya Super Min Wailer, wilayani Temeke ambako waliiba gari hilo siku moja kabla ya kukamatwa.

Mke wa Rais


Mke wa Rais Salma Kikwete(kushoto)akibadilishana mawazo na Mke wa Rais wa Marekani Laura Bush kwenye ikulu ya nchini hiyo The White House alipomtembela Laura jana.Rais Kikwete na Mkewe wapo nchini Marekani kwa Mwaliko Rasmi wa Rais George Bush.

RAIS SAMIA AKUTANA NA WAZEE WA MIKOA YOTE NCHINI, AFUNGUA UKURASA MPYA WA MAZUNGUMZO YA KITAIFA

  Dodoma, Agosti 27, 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na wazee wa Mkoa wa Dodoma pam...