VIDEO: Maombolezo ya kitaifa ya wanafunzi wa Lucky Vicent, Arusha

May 8, 2017 Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewaongoza waombolezaji ambao walikusanyika katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid, Arusha kuomboleza vifo vya watu 32 wakiwemo wanafunzi wa Lucky Vicent waliofariki katika ajali ya gari.
May 6, 2017 kulisambaa taarifa za ajali na picha zikionesha Basi dogo lililobeba Wanafunzi likiwa limepata ajali kwenye eneo la Mlima Rhotia, Karatu Arusha ambapo Kamanda wa Polisi Arusha Charles Mkumbo alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Ajali hiyo iligharimu maisha ya watu 32 akiwemo Dereva kwenye kundi la watu wazima watatu, na Wanafunzi 29 wakiwemo Wavulana 12 na Wasichana 17.
Unaweza kutazama kwa kubonyeza play hapa chini…

Comments