Monday, May 22, 2017

PSPF YATOA SEMINA KWA MAAFISA WA POLISI WANAWAKE KWENYE MKUTANO WA SHIRIKA LA MAJESHI YA POLISI KUSINI MWA AFRIKA SARPCO


Afisa mwandamzi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Delphis Richard, (kushoto), akitoa mada iliyoelezea faida mbalimbali amzipatazo mwanachama wa Mfuko huo kwa washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya maafisa polisi wanawake wa Shirikisho la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika, (SARPCO) kwenye ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es Salaam


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAAFISA wa polisi waliokuwa wakishiriki mafunzo ya siku tatu ya polisi Wanawake kutoka Shirikisho la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika, (SARPCO), wamepata fursa ya kuelewa kwa undani huduma zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia mada mbalimbali zilizotolewa na Maafis wa Mfuko huo mwishoni mwa mafunzo hayo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Maafisa hao waliokuwa wakiongozwa na Mkuu wa Idara ya Uchunguzi wa Kisayansi, (Forensic Bureau), ya Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi, (CP), Elice Mapunda walipata fursa ya kujua uendeshaji wa Mfuko huo ambao wanachama wake ni pamoja na Watumishi wote wa Umma, Sekta binafsi, na watu wote walio katika sekta isiyo rasmi.
Afisa Uendeshaji Mwandamizi wa PSPF, Bi.Amina Mtingwa, aliwaambia maafisa hao wa polisi kuwa, pamoja na kutambua na kusajili wanachama, kukusanya michango na kutunza taarifa za michango ya wanachama na kuweka michango katika vitega uchumi mbalimbali.
Alisema, majukumbu mengine ni pamoja na kulipa mafao kwa wanaostahili kwa mujibu wa sheria, kutunza kumbukumbu za wanachama na wastaafu, kuangalia upya ubora wa mafao na kufanya tathmini ya Mfuko na kuweka mikakati.
Aidha kwa upande wake, Kaimu Meneja Matekelezo wa PSPF, Bi.Ritha M.Ngalo, yeye alizungumzia mwongozo wa ujumuishaji wa michango (totalization and period of contribution guidelines 2013) kama ulivyofanyiwa marekebisho kwa polisi waliochangia GEPF na PSPF.
Aidha Maafisa hao wa PSPF, walioongozwa na Meneja Huduma kwa Wateja, Bi. Leila Maghimbi, waliweza kutoa huduma za kuwabadilishia vitambulisho na kuwapatia vitambulisho vipya baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo, lakini pia maelezo uhusu Mafao yatolewayo na Mfuko katika mpango wa uchangiaji wa lazima, ambayo yamegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Mafao ya huduma za Muda Mfupi kama vile fao la Uzazi. “Katika kujali ustawi wa wanachama wetu, Mfuko unatoa fao la uzazi kwa mwanachama mwanamke anapojifungua na dhumuni kubwa ni kumuwezesha kujikimu kimaisha wakati wa likizo ya uzazi.” Alisema Bi.Leila Maghimbi.
Fao la Mkopo wa Elimu, Fao la Kujitoa, lakini pia PSPF hutoa Mkopo kwa mwajiriwa mpya ili kujipanga kimaisha lakini faida nyingine ya anayopata mwanachama ni fursa ya kupata mikopo ya viwanja, mikopo ya nyumba, mkkopo kwa wastaafu yenye masharti nafuu.
Aidha Bi.Maghimbi alsiema, aina ya pili ya Mafao ni Mafao ya Muda Mrefu, ambayo ni pamoja na Fao la uzeeni, (Old age benefit), Fao la ulemavu, Fao la Mirathi na Fao la kufukuzwa/Kuachishwa Kazi.
Sambamba na utoaji wa mada hizo, lakini pia palikuwepo na utoaji elimu wa mtu na mtu (One to One), ambapo Bi Hawa Kikeke, ambaye ni Afisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko, alikuwa akitoa elimu kwa kukutana na mtu mmoja mmoja, huku washiriki hao waliotoka mikoa yote nchini, ikiwemo Unguja na Pemba, walipata fursa ya kuuliza utaratibu wa kupata taarifa za michango yao kwa njia ya mtandao na wengine kuchapishiwa nakala na kuondoka nazo.
Meneja Huduma kwa Wateja, Bi. Leila Maghimbi, akizungumza na washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya Maafisa wa polisi wanawake wa Shirika la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCO), kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Idara ya Uchunguzi wa Kisayansi, (Forensic Bureau), ya Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi, (CP), Elice Mapunda, (kulia), akizungumza.
 Afisa Uendeshaji Mwandamizi wa PSPF, Bi.Amina Mtingwa(kulia), akitoa mada.
Kaimu Meneja Matekelezo wa PSPF, Bi.Ritha M.Ngalo, akitoa mada
 Afisa Mwandamizi wa PSPF, Bw. Delphis Richard, (kulia), akimuonyesha Mwanachama huyu michango yake
  Mkuu wa Idara ya Uchunguzi wa Kisayansi, (Forensic Bureau), ya Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi, (CP), Elice Mapunda(kushoto), akimsikilzia Afisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko huo, Bi. Hawa Kikeke.
 Afisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko huo, Bi. Hawa Kikeke, (katikati), akiwaelekeza namna ya kutumia mtandao wa simu kujipatia taarifa mbalimbali za Mfuko.
 Mwendesha mashtaka wa polisi kutoka mkoani Mwanza, Doroth Thomas, (kulia), akiuliza maswali kuhusu michango yake kwa Afisa huyu wa PSPF
Afusa wa PSPF, akiwahudumia wanachama hawa kupata taarifa za michango yao
 Afisa wa PSPF, akitoa ufafanuzi kwa wanachama hawa wa Mfuko huo ambao ni maafisa wa polisi
  Wasirki wakifuatilia kwa makini

 Wasirki wakifuatilia kwa makini

 Washiriki wakinakili masuala muhimu yaliyokuwa yakizungumzwa na maafisa wa PSPF
Afisa Uendeshaji Mwandamizi wa PSPF, Bi.Amina Mtingwa(kulia), akisalimiana na Naibu Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Morogoro, D/RCO, Maria Dominic Kway, (kushoto), huku Bi. Kikeke akishuhudia
 Mkuu wa Idara ya Uchunguzi wa Kisayansi, (Forensic Bureau), ya Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi, (CP), Elice Mapunda(kushoto), Mrakibu  wa Polisi, (SP), kutoka idara ya Uhusiano wa Kimataifa Polisi Makao Makuu, Emma Mkonyi, (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na  Afisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko huo, Bi. Hawa Kikeke
 Mshiriki akisoma kipeperushi chenye taarifa muhimu za PSPF
 Afisa wa polisi akizungumza kwenye mafunzo hayo

Mkuu wa Idara ya Uchunguzi wa Kisayansi, (Forensic Bureau), ya Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi, (CP), Elice Mapunda,(watatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa PSPF.

No comments: