MPOGOLO AANZA ZIARA YA KUIMARISHA CHAMA MKOA WA DAR ES SALAAM


Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Lodrick Mpogolo, akizungumza na wanachama na Viongozi wa CCM Kata ya Manzese, wakati akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama, ambapo leo amenza rasmi katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema mapandikizi ya upinzani na masalia ya wasaliti hawatapenya kwenye uchaguzi unaoendelea ndani ya Chama kwa kuwa njama zao zimeshabainika. Kimesema kina taarifa kwamba waliotimuliwa CCM nao wanapanga safu za viongozi kwenye uchaguzi, lakini Chama kimejipanga vizuri katika kuchuja wagombea hivyo wenye nia hiyo hawatafanikiwa. 

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rodrick Mpogolo, alisema hayo jana alipozungumza na wanachama na viongozi wa Chama katika ukumbi wa CCM kata ya Manzese wilayani Ubungo,Dar es Salaam. 

Alisema kuna mapandikizi kutoka upinzani wanajipanga kugombea uongozi CCM jambo ambalo linafahamika hivyo hakuna atakayepenya na hatutaruhusu 'virusi' kwa namna yoyote ile. Mpogolo pia aliwaonya viongozi wa CCM wanaondekeza ugomvi ndani ya Chama na kuwataka wakatafute vyama vingine ambavyo ni maarufu kwa kugombana hadi kutwangana ngumi. 

Alisema katika mageuzi yanayofanyika sasa Chama hakitaruhusu viongozi wa aina hiyo kuendelea kuvuruga a mani, kuwachafua na kuwakandamiza wanachama wenzao. Mpogolo alisema viongozi wenye hulka ya ugomvi, kukandamiza wanachama ndio chanzo cha kupunguza kura za 

CCM katika uchaguzi, hivyo Chama hakipo tayari kuwavumilia. ''Viongozi hawa wanajulikana, kama hawawezi kubadilika, waende wakajiunge na vyama vingine ambavyo ni maarufu kwa kupigana. CCM tunahitaji kujenga umoja na upendo baina yetu maana ndio silaha ya ushindi, "alisema. 

Mpogolo alisema viongozi hao wameumiza wana CCM hadi wengine wakaenda upinzani jambo ambalo kwenye CCM mpya na Tanzania, hawana fursa ya kuendelea kutesa wenzao. katika hatua nyingine Mpogolo aliwataka wana CCM ambao wanamuwaza aliyekuwa Waziri Mkuu, na mgombea urais wa 

Ukawa Edward Lowassa, wasipoteze muda wao kwa kuwa huu ni wakati Rais Dk. John Magufuli. "Naona kuna watu bado wanawaza Ukawa, wengine bado wanafikiria mtu fulani. Ndugu zangu hii ni CCM mpya, hakuna Lowassa wala Ukawa. Nimepita mikoa 26,Watanzania wanasema hawataki upinzani, "alisema. 

Mpogolo alipiga marufuku uendeshaji wa vikao vya kushughulika na badala yake wafanye vikao vya kujenga Chama, na katika kipindi hiki cha uchaguzi wa CCM, wajielekeze kuchagua viongozi bora wasiotokana na rushwa. Alisema CCM inatakiwa kuwa mfano katika kudhibiti rushwa na kujenga nidhamu kwa viongozi na wanachama, ili iendelee kuwa kimbilio la wanyonge na Watanzania kwa ujumla. 

Mpogolo alisema Chama kina kazi ya kukomboa majimbo ya Dar es Salaam yaliyokwenda upinzani, hivyo uchaguzi ndani ya hama unapaswa kufanyika kwa umakini mkubwa ili kupata safu za viongozi wa CCM watakaofanya kazi ya kumaliza upinzani. 

Kabla ya kuzungumza na viongozi hao Mpogolo, alikutana na viongozi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam kabla ya kukutana na kamati ya siasa ya Wilaya ya Kinondoni na Ubungo ambako alipatiwa taarifa ya Chama ikiwemo maendeleo ya uchaguzi katika ngazi za mashina. 

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Lodrick Mpogolo, akisalimiana na Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu UDSM, wakati alipowasili Kata ya Msasani Tawi la Mikoroshini leo jioni akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama, ambapo jana amenza rasmi katika Mkoa wa Dar es Salaam. 

Baadhi ya wanachama wakifurahia maneno yaliyokuwa yakiongewa na Mpoglo. 

Mpogolo akipunga mikono kuwaaga wanachama

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Lodrick Mpogolo, akizungumza na wanachama na Viongozi wa CCM Kata ya Msasani Tawi la Mikoroshini, wakati akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama 

Mpogolo akizungumza na wanachama. 

Wanachama wa Msasani 

Mpogolo akiagana na wanachama baada ya kumaliza kuhutubia. 

Comments