Wananchi wakishuka katika daladala inayofanya safari zake Kibamba , Kimazichana na Dar es Salaam kwa ajili ya kuvuka kutokana na barabara hiyo kukatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Vijana wakitengeneza barabara ya dharula kwa ajili ya kupitisha magari na kupata kipato kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Picha zote na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
Barabara ya Mkuranga kwenda Hoyoyo ikiwa imekatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Diwani wa Kata ya Tengerea, Shaban Manda akizungumza juu ya barabara hiyo kukatika na kukatika kwa mawasiliano.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Kutokana na mvua zinazoendelea katika maeneo tofauti barabara mbili zimekata mawasiliano na kufanya baadhi huduma za kijamii kushindwa kufanyika.
Barabara zilizokata mawasiliano ni barabara ya Chamanzi kwenda Kibamba pamoja na barabara ya barabara ya Mkuranga kwenda Hoyoyo.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Dodoma, Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amesema kuwa hali ya barabara katika jimbo lake ziko katika hali mbaya kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Amesema kuwa ameomba barabara ya Kimazichana kwenda Kibamba kuingizwa katika barabara za Tanroads ili ziweze kuangaliwa kutokana umuhimu wake katika uchumi wa nchi.
Diwani wa Kata ya Tengerea , Shaban Manda amesema kuwa barabara ya Mkuranga kwenda Hoyoyo makaravati yaliyowekwa hayawezi kuhimili mvua ikiwa kubwa.
Amesema wakandarasi wanatakiwa kushirikisha wananchi katika uwekaji wa madaraja na makaravati kutokana na wao ndio wanajua sehemu zenye matatizo.Manda amesema kuwa wakati mwingine sehemu zinazowekwa makaravati hayana umuhimu ndio maana mvua zikinyesha nayo yanakwenda na maji .
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kimazichana , Omary Ndeu amesema hali mbaya kwa wananchi wa Mbezi na Kibamba hawawezi kufika kimazichana ambapo huduma za kijamii na biashara ndio zinafanyika
Comments