Waziri wa Viwanda,Biashara naUwekezaji Mhe. Charles Mwijage kulia akipokea cheti cha chanjo cha kimataifa kijulikanacho kama cheti cha homa ya manjano kutoka kwa Afisa Afya Bw. Fadhili Kilamile mara baada ya kupata chanjo hiyo leo kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Zungu wa kwanza kulia akisubiria kupewa cheti cha chanjo cha kimataifa kijulikanacho kama cheti cha homa ya manjano kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengocha Afya Mipakani Bw. Remidius Kakulu kushoto mara baada ya kupata chanjo hiyo leo kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma.
MbungewaVitiMaalumjimbo la SingidaMhe. Martha Mlatawa kwanza kuliaakiandikiwacheti cha chanjo cha kimataifakijulikanachokamacheti cha homayamanjanokutokakwa Afisa Afya Agnes Shirima katikatimarabaadayakupatachanjohiyoleokwenyeviwanjavyabungemjini Dodoma aliyesimamani Afisa Habari wa WizarayaAfya Bi. Catherine Sungura.
…………………………
Na.Catherine Sungura, WAMJW
Dodoma
Watanzania hususan wale wanaosafiri nje ya nchi zile zenye ugonjwa wa homa ya manjano wanatakiwa kujitokeza kwenye vituo vilivyoainishwa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kwa ajili ya kupata chanjo hiyo pamoja na kubadilisha vyeti vipya.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage wakati alipofika kupata huduma ya chanjo ya homa ya manjano ambayo inatolewa bungeni hapa
Waziri Mwijage amesema duniani ugonjwa huu upo na zipo nchi nyingi ambazo zimepoteza wananchi wake kwa kuugua ugonjwa huo“Suala hili ni muhimu sana kwa afya zetu,pamoja na kwamba nchi yetu haina mgonjwa wa homa ya manjano
Aidha amesema maambukizi ya ugonjwa huu endapo mtu ataupata gharama za matibabu yake ni ghali sana na inaweza kupelekea kupoteza maisha,hivyo ni vyema kujitokeza kwa wingi kupata chanjo hiyo pamoja na kubadilisha kadi zao kwani usiweke reheni maisha yako
Hata hivyo aliwatahadharisha wafanyabiashara,wanafunzi wale wanaosafiri au kusoma nje ya nchi ni vyema wahakikishe wanapata chanjo hiyo kuliko kupewa kadi kwa njia nyingine kwani kadi hizi zimeboreshwa na zina alama za siri ambazo nchi za kimataifa zina uwezo wa kusoma alama zetu.
Naye Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe.Mussa Zungu ameipongeza Wizara ya Afya,maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto kwa kubadilisha kadi hizi mpya kwa kuepukana na vyeti vingi ambavyo vilikua vinanunuliwa mtaani bila kupata huduma za kupata chanjo,hivyo ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanapata chanjo hizo kwani ilikua ni hatari sana hususan nchi zile zenye milipuko wa homa za manjano na hivyo kupata vyeti ambavyo ni halali
Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto limeongeza muda wa kubadilisha vyeti vya zamani hadi mwisho wa mwezi huu na baada ya hapo vyeti vya zamani havitatambulika tena.
Comments