Wednesday, May 10, 2017

SERIKALI KUBORESHA KIWANGO CHA VYOO BORA KUFIKIA 2025.

Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wa kwanza kulia akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa kampeni ya yautunzaji wa mazingira ijulikanayo kama “NIPO TAYARI”uliofanyika mjini leo mjini Dodoma. 


Waziri wa Afya, maendeleo yaJamii, jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akiwa amebeba nembo inayoashiria uzinduzi wa kampeni ya kutunza mazingira ijulikanayo kama “NIPO TAYARI” uliofanyika mjini Dodoma , wengine ni wadau mbalimbali wa mazingira pamoja na baadhi ya wabunge. 
Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza mbele ya wabunge na wadau mbalimbali wa afya na mazingira hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa kampeni ya yautunzaji wa mazingira ijulikanayo kama “NIPO TAYARI”iliyofanyika leo mjini Dodoma.  

Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akiteta jambo na Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Suleiman Jaffo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya yautunzajiwa mazingira ijulikanayo kama “NIPO TAYARI” uliofanyika mjini leo mjini Dodoma. Pichana Ally Daud-WAMJW DODOMA.
 

Na Ally Daud-WAMJW DODOMA

SERIKALIi imedhamiria kuboresha kiwango cha vyoo bora mjini na vijijini kutoka asilimia 35 hadi asilimia 55 kufikia mwaka 2025 ili kujenga taifa lenye afya bora na lisilo na maambukizi ya magonjwa yatokanayo na uchafu wa vyoo.

Akizungumza hayo kwenye uzinduzi wa kampeni ya utunzaji wa mazingira ijulikanayo kama “NIPO TAYARI” Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali imepania kufikisha asilimia ya ubora wa vyoo mpaka kufikia 2030.

“Hatua hii itafikiwa endapo kwa pamoja tutasukuma mbele ajenda ya usafi wa mazingira kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hasa katika ujenzi wa vyoo bora,utupaji salama wa taka ngumu,upatikanaji wa maji salama kwa mikono miwili” alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa yapo mafanikio yaliyofikiwa katika kupunguza kasi ya watu kujisaidia ovyo tabia ambayo ni kisababishi cha maambukizi ya magonjwa mengi katika jamii.

Mbali na hayo Waziri Ummy alitoa rai kwa wanasiasa wenginekushirikiana na wananchi katika majimbo yao ilikusukuma kwa vitendo ajenda ya Usafi wa Mazingira nchini .

Kwa upande wake Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Suleiman Jaffo amesema kuwa watanzania wa wa mijini na vijijini wawe mstari wa mbele katika kuhakikisha wanatumia vyoo bora kila kaya ili kuepuka magonjwa ya kuambukiza.

Naye Naibu Waziri wa maji na umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe amesema kuwa ili kuendana na kasi hiyo wamejipanga kuhakikisha shule zote za msingi na sekondari nchini zinapata maji safi na salama kwa wakati sahihi.

No comments: