Tuesday, May 09, 2017

Upelelezi kesi ya Masogange wakamilika


Na Karama Kenyunko,blogu ya jamii.

Baada ya mahakama kutoa hati ya kukamatwa Video Queen Agnes Gerald maarufu kama Masogange (28) kwa kushindwa kutoka mahakamani mara kadhaa, hatimae leo amejisalimisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mapema mwezi uliopita, mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilitoa amri ya kukamatwq kwa mshtakiwa Masogange kwa kushindwa kuhudhuria mahakamani mara mbili katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili.

Hatua hiyo ya kutaka kukamatwa kwa Masogange ilikuja baada ya upande wa mashitaka katika shauri lililopita, kuomba mahakama hiyo kutoa hati ya kumkamata kutokana na mshitakiwa huyo pamoja na wadhamini wake kutofika mahakamani, licha ya kupewa onyo.

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri alikubali maombi hayo na kutoa hati ya kumkamata mshtakiwa ambaye ni Masogange.

Hata hivyo, Masogange amefika mahakamani hapo leo mapema na alipoulizwa na Hakimu Mashauri sababu za kumfanya yeye kutofika mahakamani, amedai kuwa alifika lakini alichelewa.

Wakilli wa serikali Shadrack Kimaro, ameieleza mahakama kuwa upelelezi katika kesi hiyo umekamilika na ameiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea mshitakiwa maelezo ya awali(PH).

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 13 mwaka huu kwa ajili ya PH.
Awali ilidaiwa kuwa,Masogange anakabiliwa na tuhuma za kutumia dawa za kulevya aina ya heroin diacety na Oxazepam.

Awali ilidaiwa kuwa, kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu, maeneo yasiyofahamika jijini Dar es Salaam, Masogange alitumia dawa za kulevya aina ya heroin (diacety/morpline) kinyume na sheria.
Aidha anadaiwa, kutumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam
Post a Comment