WATUMISHI WOTE WA SERIKALI ZINGATIENI UHADILIFU KATIKA KAZI


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitembelea Mradi wa umwagiliaji katika kijiji cha Jobag wilaya ya Karau ,mradi uliojengwa kwa ufadhili wa shirika la Worl Vision

Na Woinde Shizza,Arusha.

Watumishi wote wa Serikali wametakiwa kuzingatia uadilifu na uwajibikaji katika utendaji wao wa kazi.

Hayo yameelezwa na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa Jana alipokuwa akiongea na watumishi wa wilaya na halmashauri ya Monduli Mara baada ya kuzindua wodi ya mama wajawazito ya hospital ya wilaya ya Monduli.

Aliwataka watumishi wote wa serikali kuzingatia uwadilifu,uwaminifu na uwajibikaji katika utendaji wao wa kazi ili dhana ya hapa kazi tu ichukue sehemu yake.

Majaliwa alisema Serikali ya awamu ya tano niyawawajibikaji,waadilifu katika sekta za umma .Amewataka watumishi wawasikilize,wawahudumie na kuwatumikia wananchi bila yakuweka ubaguzi wa aina yoyote ile.

Hii itasaidia kuonyesha matokea bora ya kila mtumishi kulingana na taaluma aliyonayo nakupelekea kuongeza ufanisi zaidi serikalini.Aidha amewataka viongozi wa halmashauri kusimamia fedha za miradi ya maendeleo zinazopelekwa na serikali na zikafanye shughuli ambazo zilipangiwa.

"Kila sekta katika halmashauri ihakikishe inapanga majukumu yake nakuyatekeleza kadri inavyopaswa"alisema Majaliwa.Aidha aliwataka wananchi kote nchini iwapo atataka Huduma n a kuhudumiwa vibaya asisite kutoa taarifa katika vyombo husika.

"Mwananchi yeyote ambae atapewa huduma vibaya na mtumishi wa serikali asisite kutoa taarifa sehemu husika ili mtumishi huyo aweze kuchukuliwa hatua Kali"alisema majaliwa.

Comments