Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya (kushoto), akihutubia wakati akizindua Baraza la tatu la Wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD), Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi MSD, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakielezwa na viongozi wao katika mkutano huo.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakiwa kwenye
mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya amewaasa watumishi wa Bohari ya Dawa (MSD) kuhakikisha kuwa wanatekeleza majukumu yao ipasavyo ili kupunguza malalamiko ya wananchi juu ya ukosefu wa dawa.
Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo Dar es Salaam leo wakati akizindua Baraza la tatu la Wafanyakazi la Bohari ya Dawa (MSD) ambapo pia amesisitiza kuwa Baraza hilo libuni mbinu na mikakati mbadala za kuboresha utendaji bila kusahau kutii miiko ya utumishi wa umma.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi MSD, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu amemweleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kuwa tayari MSD imeanza kununua dawa na vifaa tiba kutoka kwa wazalishaji, ambapo hadi sasa wanawazalishaji 20 ambao wanamikataba, na wazabuni wengine 76 wadawana 79 wa vifaa tiba zabuni zao zinaandaliwa.
Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe kutoka Makao Makuu ya MSD na Kanda zote nane za MSD ambao ni pamoja na Mwenyeviti wa Tughe na matawi pamoja wawakilishi wa wafanyakazi.
Comments