Tuesday, December 06, 2016

TANGAZO LA KAZI MRADI WA AJlRA YA DHARURA KATlKA SEKTA YA AFYA

uhuruggggggggggggggggg


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepata kibali cha mpango wa Ajira ya dharura kwa wataalamu wa “fani za Tabibu na Wauguzi. Mpango huu utaendeshwa chini ya mradi, kwa ufadhili wa fedha za Mfuko wa CDC, Award No. 5U2GGH001062-03 kwa muda wa miaka miwili.
Mradi utaajiri watumishi 192 ambao watapangiwa kufanyakazi kwenye halmashauri za wilaya 40 zenye uhaba mkubwa wa watumishi wa kutoa huduma za afya hasa kwa waathirika wenye virusi vya UKIMWI. Watumishi hawa watalipwa mishahara na stahiki nyingine kwa kufuata taratibu na kanuni za serikali. Watumishi wanaotakiwa ni Tabibu Wasaidizi (Clinical Assistant) 95 wenye ngazi ya Astashahada (Certificate in Clinical Medicine) na Wauguzi (Enrolled Nurses) 97 wenye ngazi ya Astashahada (Certificate in Nursing and midwifery).
Wizara inakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa watanzania wenye sifa zilizotajwa hapo juu, wawe na cheti cha kumaliza kidato cha nne pamoja na cheti cha taaluma aliyosomea kutoka kwenye chuo kinachotambuliwa na serikali. Barua ya maombi ioneshe wilaya ambayo mtumishi atapenda apangiwe kufanyakazi kati ya wilaya zilizopendekezwa hapo chini. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 14/12/2016.
Maombi yote yatumwe kwa:-

Katibu Mkuu
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
6 Samoral Machel Avenue,
S.L.P 9083,
11478, Dar es Salaam.
Tanzania
05/12/2016
Orodha ya Halmashauri za Wilaya na idadi Watumishi waliopendekezwa.
Na.MkoaHalmashauri  (Wilaya)Tabibu WasaidiziWauguzi WasaidiziJumla
1Arusha1. Arusha CC336
2Dar es Salaam2. Ilala MC336
3. Kinondoni MC336
4. Temeke MC336
3Dodoma5. Dodoma MC235
4Geita6. Geita DC224
5Iringa7. Mufindi DC336
8. Iringa MC224
6Kagera9. Bukoba DC336
10. Muleba DC224
7Kigoma11. Kigoma Ujiji MC235
8Kilimanjaro12. Moshi DC336
9Lindi13. Lindi MC224
10Mara14. Musoma MC224
15. Rorya DC224
11Mbeya16. Chunya DC224
17. Kyela DC336
18. Mbarali DC224
19. Mbeya CC336
20. Mbeya DC336
21. Mbozi DC224
22. Rungwe DC224
12Morogoro23. Morogoro MC336
13Mwanza24. Nyamagana MC336
25. Sengerema DC224
14Njombe26. Njombe TC224
27. Wanging’ombe DC224
15Rukwa28. Sumbawanga DC224
29. Sumbawanga MC224
16Ruvuma30. Mbinga DC224
31. Songea MC224
17Shinyanga32. Kahama DC224
33. Kahama TC336
34. Shinyanga MC224
18Tabora35. Igunga DC224
36. Nzega DC224
37. Tabora MC336
19Tanga38. Korogwe TC224
39. Muheza DC224
40. Tanga CC336
Jumla9597192

No comments: