Wednesday, December 14, 2016

Mwanachuo Aliyejifanya Shilole Apandishwa Kizimbani

1

Thomas Lucas Magula ‘Shilolekiuno_official’ (katikati), akiwa ameshikiliwa na polisi wakati wa kupandishwa kizimbani.
Na Musa Mateja
HATIMAYE lile sakata la Mwanafunzi wa Chuo cha Bandari anayetuhumiwa kutusi watu kwa kutumia jina la Shilolekiuno_official, Thomas Lucas Magula (21) mkazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam, mapema leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni.
Sakata hilo lilizalisha vichwa vya habari mbalimbali tangu Julai 20, mwaka huu baada ya kijana huyo kukamatwa na jeshi la polisi kisha kufikishwa kwenye kituo cha Polisi Oysterbay na kufunguliwa jalada la kesi lilosomeka OB/RB/20932/2010 Lugha ya Matusi kwa Njia ya Mtandao.
2Shilolekiuno_official akiwa kwenye korido kabla ya kuingizwa kwenye chumba cha mahakama.
Leo, majira ya saa 4:30 asubuhi, mtuhumiwa Magula, alifikishwa katika mahakama hiyo, ilipofika saa 8:15 mchana, alipandishwa kizimbani kisha kesi yake namba 7 ya mwaka huu, ilisomwa mbele ya Hakimu Boniface Lihamwike.
3…akitolewa mahakamani baada ya kesi yake kusikilizwa.
Akisomewa shitaka lake, mtuhumiwa aliambiwa ametenda kosa kwa kutumia lugha za matusi kisha kuchapisha habari za uongo na uzalilishaji kwa Zuwena Mohamedi ‘Shilole’, kwa njia ya kompyuta na kuziweka kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram, ambapo mtuhimiwa alikana shitaka hilo.
4…akipelekwa chumba cha mahabusu, tayari kwa kuelekea katika Gereza la Segerea.
Hakimu Lihamwike aliahirisha kesi hiyo, hadi Desemba 20, mwaka huu, huku mtuhumiwa akipewa nafasi ya kupeleka wadhamini wawili watakao mdhamini kwa shilingi mil.2 kila mmoja, ambapo wadhamini walikosekana na mtuhumiwa huyo kupelekwa lumande.
Post a Comment