Thursday, December 01, 2016

MAABARA YA KISASA YA KOMPYUTA YA SHULE YA SEKONDARI MIKOCHENI YAZINDULIWA

 Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akimuuliza jambo mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mikocheni aliyekuwa akitumia kompyuta baada ya ufunguzi rasmi wa Maabara ya kisasa ya kompyuta ya Shule hiyo, Dar es Salaam juzi. Kushoto kwake ni Meya mpya wa Manispaa hiyo, Benjamin Sitta.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta na Meya Mstaafu wa Manispaa hiyo, Yusuf Mwenda (kushoto) wakimtazama mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mikocheni, Jamila Msami akitumia kompyuta baada ya ufunguzi rasmi wa Maabara ya kisasa ya kompyuta ya shule hiyo kwa ufadhili wa Kampuni ya intaneti ya Raha Broadband, Dar es Salaam juzi.
 Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maabara ya kisasa ya kompyuta ya Shule ya Sekondari Mikocheni, Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya intaneti ya Raha Broadband, Aashiq Shariff na Meya mpya wa Manispaa hiyo, Benjamin Sitta.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maabara ya kisasa ya kompyuta ya Shule ya Sekondari Mikocheni, Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Meya Mstaafu wa Manispaa hiyo, Yusuf Mwenda.
Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kushoto), Meya mpya wa Manispaa hiyo, Benjamin Sitta (wa pili kulia), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Raha Broadband, Aashiq Shariff (wa pili kushoto) na Diwani wa Kata ya Mikocheni, Bethel Kimei (Mama Langa).


Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda ameitaka jamii kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli za kuboresha Sekta ya elimu kwa kuchangia maendeleo ya elimu ili kuleta mabadiliko ya elimu nchini.

Meya huyo Mstaafu ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Maabara ya kisasa ya kompyuta ya Shule ya Sekondari Mikocheni, Dar es Salaam kwa udhamini wa kampuni ya intaneti ya Raha Broadband kwa kushirikiana na yeye mwenyewe hivi karibuni.
Hiyo inakuwa ni miongoni mwa Maabara chache bora za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini kwa shule za Umma.
Mwenda aliutaka uongozi wa shule hiyo kuitunza maabara hiyo na kuitumia vizuri ili faida yake ionekane kwenye matokeo ya mitihani ya shule hiyo.
"Tukubaliane kuwa mtaitunza maabara hii vizuri ili umuhimu wake uonekane katika matokeo ya mitihani ya wanafunzi". Alisema Mwenda.
Aidha aliishukuru kampuni ya Raha Broadband kwa kuchangia kompyuta na vifaa pamoja na huduma ya intaneti kwa kila mwezi vyenye thamani ya shilingi milioni 18 na kuwataka viongozi wa Manispaa hiyo kuwashawishi wananchi nao kuchangia maendeleo ya elimu kwa shule za Manispaa hiyo.
Kwa upande wake Meya huyo Mstaafu alichangia shilingi milioni 3.9 ikiwa ni ukarabati wa Chumba cha maabara, madirisha, milango pamoja na meza za kompyuta.
Naye Meya mpya wa Manispaa hiyo, Benjamin Sitta alimshukuru Meya huyo Mstaafu pamoja na kampuni ya Raha kwa mchango wao na kuomba waendelee kumsaidia kwa shule nyingine za Manispaa hiyo.

Post a Comment