Friday, December 23, 2016

WAZIRI NAPE NNAUYE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA MWANAHABARI MPOKI BUKUKU

index

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa wapiga picha pamoja na Wanahabari wote nchini kufuatia kifo cha mwanahabari na mpiga picha Mpoki Bukuku kilichotokea leo katika Taasisi ya Mifupa (MOI)
Mhe. Nape Nnauye pamoja na watendaji wa Wizara wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mwanahabari huyo kwani ni pigo katika tasnia ya habari nchini.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mwanahabari Mpoki Bukuku. Kifo chake ni pigo katika tasnia ya habari hususani katika picha , nimehuzunishwa sana kwa sababu Marehemu wakati wa uhai wake ametoa mchango mkubwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo magazeti ya  Majira, Business Times , The Guardian , Nipashe na Mwananchi na The Citizen.”
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina
Imetolewa na Idara ya Habari(MAELEZO)
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Dar es Salaam
23 Desemba, 2016

No comments: