Friday, December 09, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA SHEREHE ZA MIAKA 55 YA UHURU WA TANZANIA BARA KATIKA UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi waliojitokeza katika sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi waliohudhuria sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati wimbo wa Taifa ulipokuwa ukipigwa uwanjani hapo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride katika sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Vikosi mbalimbali vya Majeshi vikipita mbele ya mgeni Rasmi kwa mwendo wa pole na Haraka katika sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Maadhimisho cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania kikionesha gwaride la kimyakimya mbele ya Amiri Jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Uhuru. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mama Fatma Karume mara baada ya kumaliza kuhutubia katika uwanja wa Uhuru.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi katika uwanja wa Uhuru mara baada ya kumalizika kwa sherehe hizo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembea pamoja na Askari Polisi ambao huongoza misafara ya viongozi VIP riders mara baada ya kuwasili Ikulu wakati wakitokea katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi mara baada ya Kuwasili katika uwanja wa Uhuru.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda mara baada ya kuwasili. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,BungeKazi,Ajira,Vijana na Wenyeulemavu Jenister Muhagama mara alipowasili katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kushiriki nkatika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara 


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na  Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  alipowasili katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kushiriki nkatika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara zilizofanyika leo
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwasili  katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kuhudhuria katika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara zilizofanyika leo


 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akikagua gwaride maalum la Vikosi vya Ulinzi na Usalama mara alipowasili katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kuhudhuria katika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara zilizofanyika leo

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akikagua gwaride maalum la Vikosi vya Ulinzi na Usalama mara alipowasili katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kuhudhuria katika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara zilizofanyika leo
Amiri Jeshi Mkuu  na Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli (katikati) akitembea kikakamavu  na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Devis Mwamunyange baada ya kukagua gwaride maalum la Vikosi vya Ulinzi na Usalama  katika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli leo Ijumaa ya tarehe 09 Desemba, 2016 amewaongoza viongozi mbalimbali na wananchi kwa ujumla katika maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara .

Maadhimisho hayo ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara yamefanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam na kupambwa na gwaride maalum lililoandaliwa kwa pamoja na Majeshi ya Ulinzi na Usalama ikiwa ni pamoja na Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ,Jeshi la Polisi,Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa.

Akizungumza na halaiki ya watanzania waliohudhuria sherehe hizo Rais Dkt Magufuli amesema mwaka jana alilazimika kuzuia kufanyika kwa shamrashamra ya maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania Bara kutimiza miaka 54 kwa kuwa alikuwa na mwezi mmoja tu tangu aingie madarakani na kuitaja sababu ya pili kuwa ni  bajeti kubwa ya shilingi bilioni nne iliyokuwa imetengwa kwa ajili ya maadhimiso hayo na kuona ni vyema ikaelekezwa katika upanuzi wa barabara ya Alli Hassani Mwinyi yenye urefu wa kilomita 4 ambayo inatumiwa na Watanzania wote badala ya fedha zile kutumiwa na wachache.

"Sherehe za miaka 55 nimeamua zifanyike kwasababu gharama zake ni ndogo sana,kwanza hakuna hata chakula baada ya sherehe hii,hakuna dhifa ya Taifa ,tukimaliza hapa tumemalizana ,lakini pili niliamua sherehe hii niifanye hapa Dar es Salaam kwa kuwa yatakuwa ni maadhimisho ya mwisho kufanyika jijini Dar es salaam na kwamba ni matumaini yake kuwa sherehe za mwaka kesho zitafanyika makao makuu ya nchia mbayo ni Dodoma"

Ameongeza kuwa sherehe za Uhuru ni tukio kubwa sana katika Taifa na hivyo serikali itaendelea kuipa umuhimu siku hiyo na kuiadhimisha.

Rais Dkt Magufuli pia amezitaja changamoto ambazo serikali ya awamu ya tano inazokumbana nazo kuwa ni pamoja na ufisadi na rushwa ndani ya baadhi ya watendaji na kuongeza kuwa mpaka sasa hivi wafanyakazi hewa wamefikia elfu kumi na tisa huku kaya masikini hewa zinazonufaika na mfuko wa TASAF zikiwa ni elfu 55 na wanafunzi hewa  mpaka sasa hivi wamefikia elfu sitini na tano.

"Serikali ya awamu ya Tano itaendelea kuchukua hatua kali ikiwa ni pamoja na kuwatumbua hadharani wale waliozoea kutumbua hadharani mali za watanzania na tuataendelea kuchukua hatua kali katika masuala ya rushwa na ufisadi,kwasababu rushwa ni saratani"
Rais Dkt Magufuli amepongeza pia jitihada zilizofanywa na watangulizi wake katika maendeleo ya Tanzania na kuwashukuru kwa niaba ya watanzania huku akiwataka watanzania wote bila ya kujali dini,itikadi za kisiasa  na makabila yao kuendelea kudumisha amani na mshikamano ili Tanzania iweze kupiga hatua za kimaendeleo kwa haraka.

"Hivyo basi tuendelee kuilinda amani yetu na kuwafichua watu wenye nia ovu ya kuhatarisha amani yetu na sambamba na kulinda amani yetu hatuna budi kudumisha umoja na mshikamano wetu ambao ni nguvu na silaha yetu kubwa kama Taifa,lakini pia tuendelee kuulinda muungano wetu ambao ni silaha kubwa ya umoja wetu ili Tanzania tuendelee kwenda mbele"

Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Dkt John Pombe Magufuli kuhudhuria na kuhutubia katika sherehe za Uhuru wa Tanzania Bara tangu aingie madarakani.


Emmanuel Buhohela
Kaimu Mwandishi wa habari Msaidizi wa Rais.
Dar es Salaam
09 Desemba, 2016.
Post a Comment