Tuesday, December 06, 2016

MATUKIO YA UHAKIKI WA WASTAAFU WANAOLIPWA NA HAZINA MKOANI ARUSHA

Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi Bw. Stanslaus Mpembe (kushoto)  akitoa ufafanuzi kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango namna zoezi zima la uhakiki wa wastaafu kanda ya kaskazini linavyokwenda kabla ya uzinduzi wa zoezi hilo. Zoezi hili ni kwa mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga. 
Zoezi la kuhakiki wastaafu likiendelea katika Ofisi za Makao Makuu, Halmashauri ya jiji la Arusha, Pichani ni baadhi ya wastaafu wakifanyiwa uhakiki.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika akifurahia jambo na baadhi ya wastaafu wanaolipwa pensheni zao na Hazina, waliojitokeza kuhakikiwa wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo katika Ofisi za halmashauri ya Jiji la Arusha, zoezi litakalo dumu kwa siku tano hadi Ijumaa wiki hii katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika akiongea na baadhi ya wastaafu waliofika katika Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa ajili ya uhakiki ambapo wastaafu hao wameiomba serikali iwaongezee kiwango cha pensheni wanacholipwa ili waweze kukabiliana na hali ngumu ya maisha.
Baadhi ya Wastaafu wanaolipwa Pensheni yao na Hazina, waliofika katika Ofisi za Makao Makuu, Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa ajili ya kuhakikiwa.
Baadhi ya Wastaafu wanaolipwa Pensheni yao na Hazina, Livingstone Kisanga (kulia) na Allen Kijazi, wakazi wa Arusha, wakisubiri kuhakikiwa katika Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Arusha, wakati wa zoezi la uhakiki wa wastaafu hao linalofanyika katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara). 
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika akihojiwa na baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali mara baada ya kuongea na wastaafu waliofika kwa ajili ya uhakiki, ambopo wastaafu wengi wameridhishwa na zoezi hili la wanashukuru zoezi hili linaenda kwa haraka kwani wengi wao wana nyaraka zote muhimu zinazohitajika.
Wawezeshaji wa zoezi la uhakiki wakibadilishana mawazo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika. Kushoto kwake ni Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi Bw. Stanslaus Mpembe na Mkaguzi wa Ndani Mkuu Bw. Paison Mwamnyasi.
Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Bw. Mohamed Mtonga, akitoa ufafanunuzi kwa wanahabari wa mkoa wa Arusha kuhusu masuala mbalimbali ya uhakiki wa wastaafu wanaolipwa na Hazina, unaoendelea katika kanda ya Kaskazini, mikoa ya Arusha, Manyara, Tanga na Kilimanjaro.
Mstaafu, Mwanakombo Yusuph, mkazi wa eneo la Kaloleni, Jijini Arusha, akihojiwa na Wanahabari mara baada ya kuhakikiwa katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha ambapo ameipongeza Serikali kwa kuendesha uhakiki huo utakaosaidia kuhuisha daftari la wastaafu na kwa uamuzi wake wa kuwalipa wastaafu kila mwezi badala ya miezi mitatu mitatu.
Bi. Amina Msigiti (kulia) ambaye ni mstaafu anayelipwa na Wizara ya Fedha na Mipango, akijiandaa kutia saini fomu yake ya uhakiki mbele ya Afisa wa Hazina, Winfrida Moshi, kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha
Post a Comment