MASAUNI KUYAFUTA MASHIRIKA YANAYOBARIKI USHOGA NCHINI, AWATAKA VIJANA KUISHI KWA KUFUATA MAADILI MEMA YA DINI

sao-1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni,  jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake Masauni aliwataka vijana kuwa makini na mashirika ambayo yanahamasisha ushoga nchini, na pia alitangaza kuyafuta mashirika hayo endapo yakigundulika. Kulia kwake ni Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Hamid Masoud Jongo.
sao-2
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia aliyekaa) akimsikiliza Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Hamid Masoud Jongo alipokuwa akizungumza na Waislam katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni, jijini Dar es Salaam leo. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo, Mhandisi Masauni, katika hotuba yake aliwataka vijana kuwa makini na mashirika ambayo yanahamasisha ushoga nchini, na pia alitangaza kuyafuta mashirika hayo endapo yakigundulika. 
sao-3
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia aliyekaa) na  Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Hamid Masoud Jongo (wapili kulia waliokaa) wakimsikiliza Shekhe wa Wilaya ya Kigamboni, Abdalla Idd alipokuwa akizungumza na Waislam katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni, jijini Dar es Salaam leo. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo, Mhandisi Masauni, katika hotuba yake aliwataka vijana kuwa makini na mashirika ambayo yanahamasisha ushoga nchini, na pia alitangaza kuyafuta mashirika hayo endapo yakigundulika.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Na Felix Mwagara (MOHA)
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amewataka vijana nchi kuwa makini na baadhi ya Mashirika yasiyokuwa ya Serikali ambayo yanajishughulisha na uhamasishaji wa mapenzi ya jinsia moja (ushoga).
Mhandisi Masauni alisema, Mashirika hayo hayapaswi kuwepo nchini kwani yanafanya kazi kinyume na mila na desturi ya nchi yetu na yanapaswa kufutwa haraka iwezekanavyo endapo yatagundulika.
Akizungumza katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni,  jijini Dar es Salaam, Mhandisi Masauni aliongeza kuwa, vijana wanapaswa wawe makini katika maisha yao, kamwe wasikubali kupotoshwa pamoja na kuendeshwa na kundi lolote ambalo linafanya kazi kinyume na taratibu za nchi.
“Kuna baadhi ya mashirika ambayo yanajihusisha kwa kutoa elimu na kuhamasisha ndoa za jinsia moja, mashirika hayo yanafanya kazi kinyume na sheria ya nchi, hivyo tunayachunguza na tukiyagundua hakuna cha Mswalie Mtume, tutayafuta haraka iwezekanavyo,” alisema Masauni.
Pia aliwataka Watanzania kutoa taarifa ya uwepo ya taasisi hizo binafsi zinazofanya shughuli hizo nchini muda wowote wakizigundua ili zifuatiliwe kwa umakini na hatimaye zifutwe haraka iwezekanavyo kwa kuwa zinaharibu jina zuri la Tanzania.
Masauni ambaye alikuwa na Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Hamid Masoud Jongo katika sherehe hiyo, licha ya kuwashukuru waandaaji wa tukio hilo kwa kumualika, pia aliwahasa Waislam nchini wawe na umoja, wapendane na waache kulalamika kwa kuwa mafundisho ya dini hiyo yanaelekeza mambo mema ambayo kila Muislam anatakiwa kuyafuata.

Comments