Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati mwenye miiwani) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Mama na Mtoto ya Chanika leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mradi ujenzi huo, Bing Hunan leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitembelea ujenzi wa hospitali hiyo leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema ndoto ya mama mmoja kitanda kimoja itatimia endapo ujenzi wa Hospitali ya Mama na Mtoto inayojengwa Chanika kwa ushirikiano wa Shirika la Maendeleo la Korea Kusini na Mkoa wa Dar es Salaam utakamilika.
Makonda alisema ujenzi wa hospitali hiyo ni muda mwafaka kwa wanawake na watoto kuwa na uhakika wa kupata huduma ya afya.
Alisema hospitali hiyo inayojengwa itahudumia watu 1000 wa nje huku vitanda katika hospitali hiyo ni 160 kwa ajili ya akina mama na watoto.
Aidha alisema wananchi waendelelee kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Pombe Magufuli ya ulipaji kodi ili nchi iwe na uwezo hata kusaidia nchi nyingine kama wanavyofanya wa Korea.
Makonda alisema madaktari watakao kwenda katika hospitali hiyo watakuwa na makazi humo ili kuondoa usumbufu wa kusafiri kila siku.
Alisema serikali inawapenda wananchi wake kuhakikisha wanapata huduma ya afya bora hususani wanawake na watoto.
Comments