Wakazi wa Kipawa walivyokutwa leo wakipanga mikakati wakati serikali ikidai iko katika hatua za mwisho za kukamilisha mchakato wa kuwalipa fidia wakazi wa Kipawa mwelekeo wa sakata hilo unatarajiwa kubadilika leo wakati wakazi hao watakapoiburata serikali mahakamani.
Kikao cha wakazi hao kilichofanyika jana Shule ya Msingi Kipawa, kwa kauli moja kilielezea dhamira yao ya kufungua kesi mahakamani kupinga serikali kutumia sheria ya zamani kwenye malipo ya fidia yao.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Evance Balama aliwahi kukaririwa na gazeti hili akisema ofisi yake na ile ya Mkuu wa Mkoa, zimeshakamilisha kazi ya kuweka saini kwenye nyaraka za malipo hayo na kuzikabidhi Wizara ya Miundombinu.
Wizara hiyo ilitarajia kuziwasilisha nyaraka hizo Wizara ya Fedha na Uchumi na baadaye Wizara ya Ardhi ili kuhitimisha zoezi hilo.Geofrey Nyang’oro na Mariam Bokero.
Comments