Cassian mshindi Bongo Star Search 2009

Mashabiki wakiwa wamekolezwa na burdani.

PAschal Cassian akifanya vituuzz.

Jaji Mkuu wa shindano Madame Ritta akiwa na Master J

Kelvin Mbati

Mheshimiwa Zitto hakuachwa nyuma

MKOA wa Mwanza umezidi kung'ara kupitia sanaa mchini baada ya mshiriki kutoka mkoani humo, Pascal Cassian kuibuka mshindi katika shindano la kusaka vipaji vya waimbaji chipukizi maarufu kama Bongo Star Search ambalo fainali zake zilifikia tamati juzi usiku kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Kabla ya ushindi huo, tayari Mwanza ilikuwa imetwaa mara mbili mfululizo taji la urembo maarufu kama 'Miss Tanzania 2009' baada mwanadada Miriam Gerald kuibuka mshindi.

Hata kabla ya kutangazwa mshindi Casian alionekana kuuteka umati mkubwa wa watu waliojitokeza kushuhudia fainali hizo kiasi cha kuwafanya wainuke kila wakati katika viti vyao na kwenda kuungana naye hasa pale alipoimba kibao cha 'Shebeneza' chenye asili ya Afrika Kusini.

Kutokana na ushindi huo, Cassian aliweza kutia kibindoni fedha taslimu shilingi milioni 25 kutoka kwa waandaaji wa shindano Kampuni ya Benchmark Production .

Mbali na zawadi hiyo kutoka kwa waandaaji, mshindi huyo pia alikabidhiwa shilingi 1,500,000 baada ya kuibuka mtunzi bora wa wimbo wa ukimwi sambamba na kitita kingine cha 500,000 kutoka duka la mavazi la Mariedo Botique ambalo pia lilidhamini shindano hilo.

Katika fainali hizo zilizohusisha washiriki watano, Peter Msechu mshiriki kutoka Kigoma aliibuka mshindi wa pili na kupata kitita cha shilingi milioni 5 taslimu pamoja na ofa ya mavazi kutoka duka la Mariedo huku mshiriki kutoka Dar es Salaam Kelvin Mbati akikamata nafasi ya tatu na kukabidhiwa zawadi ya sh 500,000 pamoja na ofa ya mavazi kutoka duka la Shear Illusion.

Mshiriki kutoka Tanga, Jackson George alishika nafasi ya nne na kupata zawadi ya vocha yenye thamani ya shilingi 200,000 pamoja na ofa ya mavazi kutoka duka la Mariedo wakati mshiriki pekee wa kike aliyeingia katika hatua ya fainali, Beatrice William kutoka Mwanza alishika nafasi ya tano na kupata zawadi ya ofa ya mavazi kutoka Mariedo.

Mbali ya zawadi hizo, duka la mavazi la Marriedo pia liliwazawadia washiriki wote watano walioingia hatua ya fainali sh 500,000 kila mmoja.

Mara baada ya kutangazwa mshindi na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Simu ya Vodacom, Ephraim Mafuru, Casian aliwashukuru Watanzania kwa kumpigia kura na wadhamini Benchmark na Vodacom kwa kumwezesha kutwaa taji hilo. Habari imendikwa na
Sosthenes Nyoni.

Comments

John Mwaipopo said…
hongera zake cassian na alistahili. strategy yake ilikuwa balaa. sijui ilikuwa ni strategy au ndio bahati. grafu ya cassian ilikuwa ikipanda taratibu lakini very steadily. wakati mshiriki kama peter msechu alishajulikana kuwa mkali grafu yake ikagota ingawaje every time alikuwa anakamua ipasavyo. ni kama vile washabiki walikuwa wanajua leo ataimba vizuri. yaani peter hakuwa na jipya katika uzuri wa performance yake, kitu kilichowafanya washabiki wajisahau kumpigia kura.

hapo ndipo alipotokea cassian. kutoka nyuma alikuwa akipanda thamani kila uchao kwa kubadilika kidogo na kung'ang'ania baritone voice kidogo. his was a fusion of master J's comments and his baritone mastery. but if cassian followed Maste J 100%, he would have lost.just imagine we are not used to 'big voices' in bongo. here comes someone from mwanza who can manipulate it in even other conventional styles. we acha tu. what is more, when people realise that as the curtains of the show were close to being pulled down. hongera cassian!

wengine walikuwa wauza sura tu. but Beatrice and the other last lady are great as well.