VURUGU ziliibuka jana kati ya wakazi wa Kipawa, uongozi wa Mamalaka ya Viwanja vya Ndege na Kamati ya malipo kwa wakazi wa Kipawa baada ya wakazi ya hao kuonyeshwa viwanja hewa wanavyotakiwa kuhamia.
Kamati ya malipo ya fidia kwa wakazi hao ilitangaza juzi kuwa jana ingefanya kazi ya kushughukia kesi za mirathi kwa wakzi hao pia kuwakabidhi viwanja wananchi ambao walikuwa hawajapata viwanja vyao.
Kazi ya kulipa fidai kwa wakazi hao wapatao 1,220 wa Kipawa ilianza Oktoba 15 mwaka huu lengo likiwa kuwalipa wakazi hoa ili waweze kuhama eneo hilo ambalo limechukuliwa na serikali kwa ajili ya upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere.
Wakazi hao wapatao 300 walisafirishwa kutoka kwenye Bwalo la Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam hadi eneo la Pugu Mwakanga ambako walitarajia kwenda kukabidhiwa viwanja vyao wanavyotakiwa kuhamia mara baada ya kukamilisha utaratibu wa malipo ya fidia.
Tayari serikali imetoa notisi za siku 45 kwa wakazi hao na kwamba wanatakiwa kuwa wamaisha hama kupisha upanuzi huo wa uwanja wa Ndege pindi wanapokabidhiwa hundi zao.
Kabla ya kusafirisha kundi la watu hao mabishona makali kati ya maafisa kutoka mamlaka ya Viwanja vya Ndege na kamati ya malipo kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa walibishana kwa muda kuhusu utaratibu unaotakiwa kuitumika katika kuwakabidhi wananchi hao viwanja vyao.
Katika mabishano hayo Injiani Sechambo, William kutoka (TAA)aliwaambia wananchi hao utaratibu uliotakiwa kutumika kuwa wataanza kuwapeleka watu kwenye ameneo hayo kwa kufuata maeneo yalivyotengwa kutoka na kazi hiyo kufanywa na mthamani mmoja. Imeandikwa na Geofrey Nyang’oro.
Comments