SERIKALI imebaini kuwa zaidi ya asilimia 90 ya wananchi wanaoishi katika mikoa ambayo iko karibu na nchi jirani wanatumia vyeti vya kughushi kwa ajili ya shughuli zao mbalimbali.
Utafiti huo ambao umefanywa na wadau mbalimbali kwa kushirikiana na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini(RITA) ambapo wamebaini kuwa, wananchi hao wameghushi vyeti hivyo kwa ajili ya kupata hati ya kuzaliwa na vifo.
Akizungumza katika uzinduzi wa cheti kipya cha kuzaliwa chenye alama za usalama, uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alisema kuuwa, kutokana na hali hiyo serikali imejidhatiti kudhibiti hali hiyo.
Alisema mpaka sasa idadi ya watu wanaoishi na vyeti hivyo ni wengi, jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa wanakiuka sheria na taratibu za upatikanaji wa vyeti halali, kutokana na hali hiyo,wameandaa mkakati wa kuzunguka nchi nzima kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya matumizi ya vyeti bandia na kuwataka watafute vyeti halali kwa ajili ya shughuli zao.
“Tunajua kama kuna baadhi ya watu wanatumia vyeti bandia kwa ajili ya shughuli zao,ambavyo wamevipata kwa njia isiyo halali jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa wanavunja sheria,kutokana na hali hiyo tumeamua kubadilisha mfumo wa vyeti vya zamani na kutengeneza vya kisasa ambavyo vitatumia teknolojia na kompyuta ili kuwadhibiti watu wanaovighushi,”alisema Chikawe.
Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo vyeti vya zamani vitaendelea kutumika mpaka hapo watapopitisha sheria ya kuvibadilisha ili kila mmoja aweze kuwa na vyeti vya kisasa ambavyo ni vigumu kwa mwananchi wa kawaida kuvitengeneza.
Alisema kutokana na hali hiyo wananchi wenye tabia ya kughushi vyeti hiyo wametakiwa kuacha mara moja kwa sababu ni kos ala jinai ikiwa mtu atabainika maehusika katika zoezi zima la kughushi vyeti hivyo na kuchukulia hatua kaliza kisheria.
Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa RITA, Philip Saliboko alisema kuwa vyeti hivyo vipya vitaanza kutolewa leo katika ofisi za RITA zilizopo upanga jijini Dar es Salaam.
Comments